


Mkono
wa kulia wa Xiao Wei mkazi wa Changde, Kusini mwa China, uliunganishwa
katika kifundo cha mguu wake kwa mwezi mzima kabla ya madaktari
kuurudisha eneo lake. Mkono wa Xiao ulikatika katika ajali kiwandani
alipokuwa kazini.
"Nilishtuka
sana na kushindwa kuondoka eneo hilo mpaka wafanyakazi wenzangu
walipoondoa mashine na kutoa mkono wangu kisha kunipeleka hospitali"
Alisema Xiao, akielezea ajali hiyo iliyotokea mwezi uliopita.
Baada ya
kupelekwa katika hospitali mahiri nchini China, saa saba baada ya ajali
hiyo, madaktari walisema wataurudisha mkono huo ila siyo moja kwa moja.
Ili kuzuia mkono wa Xiao
usiharibike, madaktari waliamua kuuunganisha katika kifundo cha mguu
ambapo ulikaa kwa mwezi mzima baada ya kupona majeraha mengine ndipo
walipourudisha katika eneo lake. Madaktari wanadai Xiao atapona vizuri
na mkono wake utafanya kazi kama zamani.
(Chanzo: Metro)

No comments:
Post a Comment