MWENYEKITI wa Kamati ya Umoja wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania, Kimela Billa, ameutaka uongozi wa Shirikisho la Muziki Tanzania, kumchukulia hatua ya kinidhamu, msanii wa muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kosa la kukiuka maadili ya Tanzania katika tamasha la Serengeti Fiesta, mkoani Iringa.
Shilole
 alipanda jukwaani akiwa anacheza wimbo wake wa ‘Nakomaa na jiji’ huku 
akiwa amevaa nguo ambazo zinaonesha maumbile yake yote ya mwili.
Akizungumza
 jijini Dar es Salaam, Billa alisema Shirikisho la muziki chini ya rais 
wake, Addo Novemba wanatakiwa kuchukua hatua zaidi juu ya shilole kwa 
kosa la kuwadhalilisha wanawake ikiwa ni pamoja na kukiuka maadili ya 
Tanzania.
“Hatukatai
 hayo mambo yapo lakini kwa staili ile sisi kama viongozi wa sanaa 
hatutaweza kuvumilia, shirikisho la muziki wakishindwa kutekeleza hili 
lazima kamati ilivalie njuga swala hilo, kiukweli wanalidhalilisha taifa
 hawa wasanii, mbona wanaume hafanyi shoo zao uchi,? Alihoji Billa.
Alisema
 shirikisho la muziki liige mfano wa shirikisho la filamu kama 
lilivowaonya Wema Sepetu na Aunt Ezekiel kwa makosa kama hayo, ambapo 
anamini kwaasilimia kubwa kunachangia kuwa na nidhamu wanapopanda 
jukwaani.
“Angekua ameenda kwa shughuli za filamu wangelifanya wao lakini hili shirikisho la muziki wanatakiwa wakae meza moja na Shilole kulizungumzia hilo, wao wanakua wazito kuwachukulia hatua wasanii wa muziki kuliko filamu lakini kwa hili haitawezekana, ,” alisema
 

 
No comments:
Post a Comment