Picha
 aliyoipost mtandaoni Staa wa filamu za Kibongo,Irene Uwoya ikimuonyesha
 mtoto wake Krish Ndikumana akiwa ameshika glasi ya pombe imemfanya 
msanii huyo ashambuliwe baada ya mashabiki wake kutoa maoni kwamba 
hapaswi kufanya hivyo kama mzazi na kioo cha jamii kwani anamfundisha 
tabia mbaya mtoto wake huyo.
 
 
Irene
 amepost picha hiyo akiwa Jijini Arusha katika hoteli ya Mount Meru na 
msanii mwenzake Blandina Chagula‘Johari’wakila bata na marafiki zao wa 
huko
 
 
No comments:
Post a Comment