Kabla sijapata mimba walikuwa karibu sana na mimi tulikuwa tukienda wote club na swimming na matembezi mengine. kwasasa mimi siwezi huwa nikirudi tu kazini nakaa nyumbani sitoki tena. Mpaka huwa nafikiri labda kwasababu wanaona nina hili tumbo ndio mana wana nitenga au labda wao hawana kizazi ndio mana wananipotezea lakini sitokaa na hili tumbo milele nitajifungua na nitakuwa kama wao.
Sikumoja nilipata maneno kutoka kwa mmoja wao kuwa fulani na fulani wanasema kuwa huna jipya tena habari yako imeisha. Nilijisikia vibaya sana kusikia wanawake wenzangu wananiambia maneno kama hayo. Naombeni Ushauri Ndugu Zangu Nifanyeje
kaa kimya muombe mungu ujifungue salama na akupe mtoto atakae kusaidia baadae
ReplyDelete