Kuzaliwa: Oktoba 13, 1980  Mahali: Accra, Ghana  Klabu za 
Awali: 2000-2005:Liberty Professional   2005-2006: Pisico Binh D?nh F.C.
 ,Vietnam (mkopo)   2006-2009: Liberty Professional   2009- 
2012:         Yanga SC 
            
SIMBA imemtumia tiketi ya ndege kipa wa zamani wa Yanga, Yaw 
Berko na atatua jijini Dar es Salaam kesho Ijumaa kufanya mazungumzo ya 
mwisho na klabu hiyo ya Msimbazi.
Mwanaspoti linaweza kuthibitisha pasipo shaka kuwa
 Berko atatua kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Kenya kwa ajili ya 
kufanya makubaliano ya kuidakia Simba kuanzia mzunguko wa pili wa Ligi 
Kuu Bara unaoanza Januari 25 mwakani.
                
              
Simba imepanga kumpa mkataba wa miezi sita Berko 
ambao utakwisha Juni mwakani na kuwepo kwake kutategemeana na kanuni 
mpya za Ligi Kuu Bara kwani huenda kusiwe na makipa wa kigeni kuanzia 
msimu ujao kama kanuni mpya zitaanza kutumika.
                
              
Tayari uongozi wa Simba umempa maagizo kipa wao wa
 sasa raia wa Uganda, Abel Dhaira kumtaka atafute timu nyingine kutokana
 na kupungua kiwango pamoja na gharama kubwa.
                
              
Mmoja wa waandishi maarufu wa Ghana aliliambia 
Mwanaspoti jana Jumatano kuwa Berko amepokea tiketi hiyo na atatua 
katika ardhi ya Tanzania Ijumaa.
                
              
Berko alipopigiwa simu kuthibitisha habari hizo, 
kwanza aliguna, halafu akazungumza kwa Kiswahili; “Wewe nani? Baada ya 
mwandishi kujitambulisha na kumuuliza kuhusu suala la kujiunga Simba 
alicheka halafu akasema: ‘‘Nipigie baadaye tuzungumze nipo mazoezini.” 
Hata hivyo hakupatikana tena.
                
              
Viongozi wa Simba walionekana kushangazwa kila walipotafutwa kuthibitisha hilo, huku wengi wakisema hawana habari na hilo.
                
              
Hata hivyo, uchunguzi wa ndani wa Mwanaspoti 
unaonyesha kuwa Berko ameipokea tiketi ya ndege aliyotumiwa na Simba na 
atatua kesho Ijumaa kufanya mazungumzo na klabu hiyo ya Msimbazi.
                
              
Berko aliondoka Yanga mwaka huu baada ya klabu 
hiyo ya Jangwani kumpa dola 7,500 (Sh 12 milioni) alizokuwa anawadai 
kutokana na kuvunja mkataba.
                
              
 Yanga ilimtoa Berko kwa mkopo kwenda FC Lipopo ya
 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili wabadilishane na Mnyarwanda 
Kabange Twite, pacha wa kiraka wa klabu hiyo, Mbuyu Twite, lakini mpango
 huo ulishindikana msimu uliopita.
                
              
Baadaye kipa huyo bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 
mwaka 2011/12 alibaki Jangwani lakini bila kucheza akawa mtu wa 
kujifungia chumbani muda wote makao makuu ya Yanga.
                
              
Berko, ambaye matarajio yake ya mbele ni kuwa 
mchungaji wa kanisa alipokuwa anawaaga mashabiki wa Yanga mapema mwaka 
huu, alisema anaondoka Jangwani, lakini kuna siku watamkumbuka.CHANZO MWANASPOTI
 
 
No comments:
Post a Comment