Usaliti! Recho Mathias (23) anadai kumshika ugoni mumewe wa ndoa akiwa na mwanamke ndani ya chumba chake tena kitandani.
Tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita maeneo ya Mashiri, Mabatini mkoani hapa ambapo Recho alirejea kutoka safarini na kumkuta mumewe anasaliti ndoa yao na mwanamke mwingine aliyedai kuwa ni mke wake halali.
Habari zilidai kuwa baada ya Recho kukutana na hali hiyo chumbani kwake, moja kwa moja alitoa taarifa kwa viongozi wa serikali ya mtaa ambao walishirikiana na wanaharakati wa jinsia wa FARIJIKA na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers katika ‘kusovu’ ishu hiyo.
Kama kawaida, makamanda wa OFM walijiridhisha kwanza kama kweli mwanaume huyo ni mume wa ndoa wa Recho.
Ilibainika kuwa kweli ni wanandoa ambapo katika kipindi kifupi cha mwezi mmoja ambacho Recho alikuwa safarini kumuuguza bibi yake, mumewe alichukua mwanamke mwingine kwa makubaliano ya kufunga ndoa.
Baada ya kunasa tukio zima, OFM ikiwa sambamba na Recho, balozi wa mtaa na balozi kiongozi aliyejitambulisha kwa jina la Musa Mohamed, walifika eneo la tukio na kumshuhudia mwanamke mwingine wa mwanaume huyo aliyejitambulisha kwa jina la Salha Hassani akiwa amelala chumbani bila wasiwasi.
Salha alipoulizwa kama anatambua kuwa mwanaume huyo ana mke alishangaa na kusema kuwa hakuwa akijua chochote zaidi ya kusikia uvumi mtaani.
Huku akiwa na jazba, Recho alifunguka kuwa kinachomuumiza zaidi kuhusu mwanaume huyo siyo kitendo cha chumba chake kutumiwa na mwanamke mwingine bali ni mali ambazo wamechuma wote huku kiasi kikubwa zikiwa zake.
Naye mwanaume huyo alipobanwa na OFM alikataa.
Kuhusu madai ya mkewe kutaka kugawana mali walizochuma, mwanaume huyo alisema atajitahidi kumlipa huku akiomba suala hilo lisifike mbali badala yake apewe muda.
Hata hivyo, suala hilo lilipelekwa katika baraza la usuluhishi la serikali za mtaa ambapo Recho na mumewe wanatarajiwa kuitwa leo (Jumatatu) kwa ajili ya kusikiliza shauri lao huku taratibu za kisheria za kushikwa ugoni zikifuatia.
CREDIT: GPL
No comments:
Post a Comment