Katika
 hali isiyokuwa ya kawaida na ya kushangaza, kumemezuka tabia ya vijana 
ambao wanashinda kakika kivuko kinacho unganisha Posta na Kigamboni 
wakivizia kivuko hicho kinapopita kupanda na baadae kinapo ondoka hata 
kikifika umbali mrefu wao kuanza kuruka na kupiga mbizi.
Mtandao
 huu wa Dar es salaam yetu umekuwa ukifuatilia kwa kina swala hili na 
kigundua kuwa hakuna mtu ambaye anawazuia vijana hawa wanaofanya mchezo 
wa hatari, ingawa kwa upande wa pili kimekuwa ni kivutio kikubwa kwa 
wale wasafiri..
Vijana
 hawa ambao hawalipii hata kiasi kidogo katika kivuko hicho wameendelea 
kuhatarisha maisha yao na pindi wakijua na kufahamu kabisa eneo ambalo 
kivuko kinapita huwa ni sehemu ndefu sana ambayo inaweza kusababisha 
madhara makubwa kwao na pengine kifo.
Hata hivyo inawezekana wahusika hawalijui hili au lah wanalijua lakini hawalizuii, hili ni jambo letu sote kujiuliza.
Tazama sasa hapa kinacho tokea.....  
 Pichani
 ni Kijana ambaye alionekana anaruka kutoka Juu ya Pantoni(Kivuko) Mbele
 kidogo baada ya Pantoni hiyo MV. Magogoni kuanza safari zake, huku 
abiria wangi wakiwa wameacha viti vyao na kuendelea kushangaa.
 Wakati huo huo Kijana mwengine nae alionekana anachomokea kutoka katika Pantoni hiyo na kuzamia majini 
 Wasafiri
 walipigwa Butwaa zaidi kuona kasi ya vijana hao inazidi kuongezeka na 
huyu kijanda ndiye aliyekuwa anafunga dimba la kuzamia majini.
 Hapa
 ni Baada ya vijana hao kuzamia majini na wengine hawaonekani 
yanaonekana maji tuu yanaruka wakati wao wapo chini ya maji hayo.
Ni
 zaidi ya Vijana 9 ambao wote walipanda Pantoni hiyo ya MV.MAGOGONI bila
 ulinzi wowote na baadae kupiga Mbizi wakitokea katika Pantoni hilo... 
 
 
No comments:
Post a Comment