KAMA HAUKUJUA BASI JUA:
Hata UBONGO unaweza kufanyishwa mazoezi ili kuuongezea uwezo wa kufanya kazi na matunzo kama tunavyofanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya
miili yetu. Hata hivyo mazoezi ya ubongo yapo tofauti kama vile:-
=>Michezo ya kompyuta (computer games) hususani games maalum zinakutaka ufikirie na kufanya maamuzi kwa haraka na games zinahitaji uwe na kumbukumbu ya haraka, na game zinakufanya upangilie mikakati ya kushinda kama MAZE GAME.
=>Michezo ya kawaida: Huzoesha ubongo wako kuwa makini kwa kuwa kuna kitu unachofanya kinachohitaji ubongo wako kuwa makini.
=> Jifunze kitu kipya: Wataalamu wanasema hata kujifunza lugha mpya huongeza uwezo wa ubongo kufanya kazi.
=> Kuwa na muda wa mara kwa mara wa ukimya ili kufanya ubongo wako utulie na 'kupangilia' taarifa.
=> Ok. Mazoezi ya kawaida nayo yamo. Wataalamu wa Ohio University wa huko Marekani wametaja hili.
 
 
No comments:
Post a Comment