
Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuanza mara moja mpango mkubwa wa ujenzi wa kimataifa wa reli ya kati baada ya kupatikana kwa mafanikio makubwa ya ujenzi wa miundo mbinu ya barabara kwa kiwango cha lami nchini kote.
Mh
 rais kikwete ametangaza mpango huo mkubwa wa ujenzi wa reli ya kati kwa
 kiwango cha kimataifa,wakati akihutumia maelfu ya wananchi wa mji wa 
Old Maswa wilayani Bariadi mkoani Simiyu muda mfupi kabla ya kuweka jiwe
 la msingi kwa ujenzi wa barabara ya kilometa  71.7 inayojengwa na 
kampuni ya cc ya nchini China kwa kutumia fedha za ndani kiasi cha 
shilingi bilioni 70.
Hata
 hivyo rais Kikwete,amesema serikali,imekuwa ikitumia fedha nyingi 
katika ujenzi wa miundombinu ya barabara yakiwemo madaraja ili kuchochea
 kasi ya ukuaji wa uchumi, huku akisema kati ya madaraja makubwa matano 
yalipangwa kujengwa baada ya uhuru,rais wa kwanza Mwl Julius Nyerere 
ameweza kujenga daraja la Kirumi mkoani Mara na rais  wa awamu ya tatu 
Benjamin Mkapa amejenga daraja la mto Rufiji na sasa serikali yake 
imekamilisha ujenzi  wa madaraja matatu yaliosalia.
 
 
No comments:
Post a Comment