![]() |
| Chuchu Hans |
RJ Company chini ya Blandina Chagula(Johari) na Vicent Kigosi(Ray)
wanakuja na filamu mpya ya Love Maniac na hii ni exclusive news ambayo Blog ya swahili planet
imeipata kutoka kwa chanzo makini kilicho karibu na watengenezaji wa
filamu hiyo.
![]() |
| Muonekano wa Ray katika filamu ya Love Maniac...... |
Kama hivi karibuni umeona Ray akiwa na tattoo nyingi
mwilini na nywele za blond basi ni kwa ajili ya character yake katika
filamu hii ambapo amecheza kama kijana wa kisasa na mhuni. Muigizaji
mkuu wa kike wa filamu hii ni Chuchu Hans ambaye anapendwa sana
kimapenzi na kijana mstaarabu ambapo nafasi hiyo imechezwa na Walter De
Ngonde lakini Chuchu hapendi wanaume na hamtaki kabisa Walter ambaye
anafikia hatua anawatumia wazazi wake(Mzee Masinde) wamsaidie kumpata
Chuchu lakini mwishowe Chuchu anaangukia kimapenzi kwa kijana mhuni
mwenye tattoo nyingi mwilini ambapo nafasi hiyo imechezwa na na Ray na
hatimaye Chuchu anakuwa kichaaa kutokana na issues za mapenzi. Mastaa
wengine katika filamu hiyo ambayo bado inashutiwa kwasasa ni Kupa.


No comments:
Post a Comment