Pichani ni baadhi ya wafu waliofukuliwa kaburini na kuvishwa nguo
Indonesia.
KILA mwaka huko Tana
Toraja, Indonesia, wafu (au maiti) hufukuliwa kutoka makaburini ili
kubadilishwa nguo. Watu wa eneo hilo wa kabila la Toraja wana mila za ajabu
kuhusu vifo na 
maisha yanayofuata baada ya mtu kufa.
Wao mtu akifa hutakiwa
kuzikwa katika eneo alilozaliwa na si lazima azikwe katika eneo alilofia.
Idadi kubwa ya watu wa eneo
hilo ni Wakristo, wanaofuata ni  Waislam  na wengine ni Wapagani
ambao wanajulikana kwa imani  au madhehebu ya Aluk To Dolo yaani “Njia ya
Mababu”.
Torajan huishi katika
maeneo ya milimani na hawataki kujulikana sana katika jamii, japokuwa wana mila
na desturi zao zilizoenea katika jimbo la Sulawesi.
 

 
No comments:
Post a Comment