adsence

Pages

Monday, November 25, 2013

MSANII BONGO MUVI AMSHUSHIA KIPONDO MAMA MWENYE NYUMBA WAKE AMBAYE ALIKUWA ANA MIMBA..IVI NDIVYO ILIVYOKUA

Msanii wa filamu za Kibongo, Jumanne Mshindo anadaiwa kumfanyia fujo mama mwenye nyumba wake, Farida Hamisi kisha kutuhumiwa kumpiga na kumjeruhi huku akijua ana mimba.
 
Msanii wa filamu Bongo, Jumanne Mshindo.
Akizungumza na namba moja la mastaa na skendo za kijamii,  hivi karibuni, Mbagala jijini Dar, Farida alisema kuwa kisa cha kupigwa ni rafiki yake ambaye alipeleka maneno kwa mke wa msanii huyo.
“Unajua Jumanne alikuwa akinitaka nikamkataa na kumwambia mume wangu ambaye aliniambia nimdharau kwa sababu ya tamaa zake, sikuishia hapo nilimueleza rafiki yangu mmoja ambaye alipeleka maneno kama yalivyo kwa mke wa Jumanne,” alisema Farida.
Mama mwenye nyumba, Farida Hamisi.
Mwanamama huyo alisimulia kuwa baada ya maneno kumfikia mke wa Jumanne, waligombana na mumewe ambaye alikasirika na kwenda kumpa kipigo kilichomsababishia maumivu makali kwa kuwa ni mjamzito.
“Alipomaliza kunipiga alikimbilia Kituo cha Polisi Mbagala, Dar wakaja kunikamata,” alisema kwa masikitiko.
Alidai kuwa polisi walipofika kumkamata walishangaa kumkuta katika maumivu makali kwani tumbo lilikuwa likimuuma kufuatia kiumbe kilichokuwa tumboni kukaa vibaya.
PF3 aliyopatiwa Farida kutoka polisi baada ya kipigo cha Jumanne.
Alisema kuwa polisi waliwachukua wote huku wakimwamuru msanii huyo kutoa fedha za matibabu baada ya kupatiwa fomu ya matibabu (PF-3).
“Jumanne alinipa elfu 30, nikaenda kutibiwa Hospitali ya Mbagala-Zakhem ambapo waliniambia nimepata maumivu na mtoto amekaa vibaya,” alisema.
Farida alisema kuwa aliamua kumfungulia Jumanne kesi ambapo alipewa RB katika Kituo cha Polisi cha Mbagala, shitaka likiwa ni shambulio la kudhuru mwili hivyo msanii huyo anasubiri kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Baada ya habari hizo kupenyezwa kwenye meza yetu, waandishi wetu waliwasiliana na Jumanne ambaye alikiri kuwa na matatizo kidogo ambayo walikwenda kuyamaliza kwa mkuu wa kituo.

-Gpl

No comments:

Post a Comment