 
 
Watu 17 wamejeruhiwa baada ya gari la 
abiria walilokuwa wakisafiria kutoka ulowa kwenda mjini kahama kuacha 
njia na kupinduka katika kijiji cha Nyandekwa wilaya ya kahama mkoani 
Shinyanga. 
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi 
ikilihusisha gari namba T 208 AGE lilokuwa likiendeshwa na dereva 
aliyetajwa kwa jina la Rashid Ramadhan mkazi wa Kahama mjini, ambaye 
hata hivyo alitoroka baada ya tukio hilo. 
Kwa mujibu wa daktari mfawidhi wa 
hospital ya wialaya ya Kahama, Deogratius Nyaga, jumla ya majeruhi 5 
wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa huku 12 wakiwa wanaendelea na matibabu
 hospitalini hapo. 
Mganga mfawidhi wa hospital ya wialaya ya Kahama, Deogratius Nyaga akiongea na waandishi wa habari 
Daktari Nyaga amewataja waliolazwa kuwa
 ni Elizabert Mgesa (49), Katarina Makoye (32), Eliza Timotheo (30), 
Ngeke Chanila (23), Zawadi Andrea (18), Amos Hussein (32) na Adam John 
(20) ambaye alikuwa kondakta wa gari hilo.  
Wengine ni Zakaria Leonce (25), Mabala 
Paulo (28), Hamis Makala (26), John Marcel (26) na Michael Rashid (47) 
na motto benad Paulo mwenye umri wa miezi mitano na kwamba wote hali zao
 zinaendelea vizuri. 
Jeshi la Polisi wilayani kahama 
limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba uchunguzi wakubaini 
chanzo chake unafanywa, huku juhudi za kumtafuta dereva wa gari hilo 
zikiendelea. 
 
 
Majeruhi akiwa na ndugu yake ambaye amekwenda kumtembelea 
 
  
  
 
Ajabu sana: Majeruhi wawili wakiwa katika kitanda kimoja 
 
 
Mama aliyejeruhiwa pia katika ajali hiyo 
 
 
Mgonjwa akiwa amepumzika baada ya kupatiwa huduma 
 
 
Miongoni mwa waliopata ajali akiwa kitandani wodini 
 
 
Dada huyu akiwa ametulia kitandani kumuomba mungu ampe ahueni 
 
 
Majeruhi wawili katika kitanda kimoja kama inanvyoonekana 
 
 
No comments:
Post a Comment