Matukio
 ya kutisha yamezidi kutikisa nchini Brazil baada ya kijana mmoja mwenye
 miaka 17 kukutwa amekufa huku panga likiwa limechomekwa katika koo lake
 huku utumbo ukiwa nnje kutokana na jeraha kubwa alilolipata tumboni.
kijana
 huyo alikutwa na mauti hayo katika nyumba ya kulala wageni iliyopo huko
 Sao Domingos, manispaa ya Brejo da Madre De Dios Nchini,Brazil tukio 
hilo lilijili siku ya Alhamisi mchana.
Polisi
 nchini Brazili wamedai kuwa kifo cha kijana huyo huwenda kikawa 
kimesababishwa na madeni aliyokuwa akidaiwa na watu mbalimbali.Mpaka 
sasa jeshi hilo linawashikilia watu wawili wanao sadikiwa kuhusika na 
tukio hilo pia Chuma cha mazoezi kilichokutwa karibu na mwili huo 
kimechukuliwa na tume ya mauaji kwajili ya uchunguzi zaidi.

Pia
 polisi wamedai kuwa kijana huyo licha ya kuwa na umri wa miaka 17 
alikuwa tayari na majarada ya kesi kibao mahakamani na moja ya makosa 
yaliyo kuwa yakimkabili kijana huyo ni kumiliki bunduki kinyume na 
sheria.




 
 
No comments:
Post a Comment