Jumamosi ya November 30, tuzo za 10 za video za Channel O 
aka CHOAMVA zilitolewa huko Kliptown, Soweto (Johannesburg) nchini 
Afrika Kusini.
Mwaka huu ni AY pekee ndiye alikuwa msanii wa Tanzania aliyekuwa 
akiwania tuzo hizo. AY alikuwa akishindania kipengele cha video bora ya 
Afrika mashariki na video bora ya msanii wa kiume Afrika.
Bahati mbaya, AY hakufanikiwa kututoa kimasomaso na P-Unit kuchukua 
tuzo ya video bora ya Afrika Mashariki. Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri 
wa Twitter, utagundua kuwa AY alikuwa akipiga kampeni ya nguvu kuwaomba 
watanzania wampigie kura. Marafiki zake, wasanii wenzake na vyombo vya 
habari vilimsaidia pia kuufisha ujumbe huo bila kuchoka.
Kampeni ilikuwa kali kiasi cha kumtia yeye mwenyewe moyo kuwa huenda 
mwaka huu angeibuka na tuzo pia na kutupa sifa Tanzania. Hata hivyo 
mambo yalienda tofauti na AY hakufanikiwa kupata tuzo.
Lakini ukweli unaouma ni kwamba, wabongo tumekuwa ni watu wa kuongea 
bila vitendo. Hakuna ubishi kabisa kuwa Watanzania wengi waliokuwa na 
uwezo wa kumpigia kura hususan kwenye internet ambako ni bure, 
hawakufanya hivyo sembuse kwa sms ambako fedha hukatwa?
Tumekosa uzalendo na kupenda vya kwetu. Badala yake tumekuwa ni watu 
wa kupuuzana na kuchukuliana poa tukiwathamini watu wa nje kuliko 
wazawa.
P-Unit hawakuwa na nguvu kama aliyonayo AY lakini wamefanikiwa 
kuitwaa tuzo hiyo kwakuwa Kenya ilikuwa nyuma yao. Tujifunze kuwa nyuma 
ya wasanii wetu pale wanapokuwa wanahitaji kura zetu kwenye mashindano 
ya kimataifa kwakuwa bila support ya nyumbani hawawezi kufika popote.
Mpaka sasa AY bado hajasema chochote lakini swahiba wake walienda naye Afrika Kusini, Mwana FA alitoa shukrani kwa niaba yake.
“Tunamshukuru kila mmoja aliyemuunga mkono @AyTanzania kwa namna 
yeyote ile kwy huu mchakato...haikuwa yetu safari hii!all good,hakuna 
malalamiko KABISA. Mapambano yanaendelea. Mwaka ujao pia kuna 
nyingine...na kuna muziki wa kuendelea kufanya..keep listening."
Naye Salama Jabir aliandika: S/O kwa mwanangu @aytanzania na kila 
mmoja alom support...kwenye macho yangu na yako naamini ni mshindi toka 
siku ya kwanza. tugange yajayo.”
Ni kweli tugange yajayo kwakuwa ni wasanii wengi tu wakubwa pia waliokosa tuzo mwaka huu.
 
 
No comments:
Post a Comment