Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono.
Kuna
watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa
uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.Mtu anaweza kuwa na mke
na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna
wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa
mahari. Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini
uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza
hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono.
Pamoja
na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na
kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema
tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika
kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya
miti kwa vile tu miili imetaka kufurahika.
Twende pamoja katika kutazama madhara hayo kwa kina.
KUPOTEZA HAMU YA TENDO.
Watu
wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa
wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza
wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara.Sababu hizo zinaweza
kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata
anapomuona akiwa mtupu.
Aidha
kukinai haraka staili za kimapenzi kunatajwa kujitokeza kutokana na
kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine sehemu
moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza kumfanya
mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye
na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.
KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA.
Tabia
ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini
na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo
la ndoa bila kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa
kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi na kwa
wakati gani?
Watu
wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndiyo wale ambao
kila wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake.Hawa
ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa watumishi wa ndani au
kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa
zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi.Unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi mara
kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa yako. Mumeo akiondoka siku
mbili unatamani kuwa hata na houseboy ili akukate kiu ya penzi.
KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO.
Raha
ya tendo hutegemea sana hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na
kiu ya kufanya mapenzi, hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila
mara unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha
ambayo haikutoshi kumaliza tamaa yako.Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya
kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo!
KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI.
Madhara
mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni
pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili.Kama tujuavyo tendo la ndoa
hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya mwili
uchoke. Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa
nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.Sambamba na hilo mbegu
za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa
dhaifu.
KUPATA MAGONJWA
.
Kama
tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa na tamaa
na hujikuta wanafanya mapenzi holela ambayo huweza kuwasababishia
magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi, lakini ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na
msukumo wa kutosha hasa kwa wanawake huwafanya waishiwe msisimko na
kuzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko
wakati wa kujamiiana na hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza
kuleta maambukizi ya haraka ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi
No comments:
Post a Comment