Simu
 hizo zina uwezo wa kujirudisha katika hali ya kawaida (self-healing) 
mara baada ya kupata mikwaruzo ya kitu chenye ncha kama funguo, kisu nk,
 na baada ya muda 
alama zote za mikwaruzo zinapotea na kurudi ilivyokuwa.
alama zote za mikwaruzo zinapotea na kurudi ilivyokuwa.
Pia
 display ya simu hizo za LG G Flex imetengenezwa kwa plastic badala ya 
kioo kama zilivyo simu zingine, na pia muundo wake wa kujikunja (curve) 
unairuhusu simu kunyooka pindi inapokandamizwa kwa nguvu na kurudi 
katika hali yake bila kuvunjika.
Kwa
 simu hizi za G Flex, mtumiaji hatapata yale maumivu ambayo huwakuta 
watumiaji wengi ya kuvunjika kwa kioo, au simu kupata mikwaruzo mingi 
inayosababisha kuifanya ichakae haraka.
GG
 Flex ambazo kwa sasa zinapatikana Korea peke yake zitazinduliwa kwa 
soko la kimataifa Jumanne ijayo (December 3) huko Hong Kong. Bei ya simu
 hizo kwa Korea ni 999,990KRW sawa na Tsh milioni moja na nusu.
Tazama video kujionea majaribio ya G Flex
SOURCE: YAHOO
 
 
No comments:
Post a Comment