adsence

Pages

Thursday, December 19, 2013

Wema Sepetu "Hakuna filamu niliyoifanya na isiwe gumzo, namshukuru Mungu na marehemu Kanumba kwani aliniona ninafaa kuwa muigizaji"




WEMA Sepetu ameweka wazi kwamba tangu aanze uigizaji filamu miaka mitano iliyopita ameshiriki filamu 10 pekee ambazo hata hivyo zimefanya vizuri.

Wema alisema kuwa anashukuru Mungu kutokana na mafanikio yaliyotokana na kazi alizozifanya kwa kipindi kirefu.

“Hakuna filamu niliyoifanya na isiwe gumzo, namshukuru Mungu na marehemu Kanumba kwani aliniona ninafaa kuwa mwigizaji na nikawa staa, unajua unapotengeneza kazi wewe mwenyewe pia unakuwa na uwezo wa kuiuza, ndiyo maana kuna watu wanachekesha unapomuona tu hata hajaongea lolote, huyu ana kipaji cha uchekeshaji,” alifafanua.

Licha ya ustaa alionao mwanadada huyo anasema hapendi kujiweka hadharani mara kwa mara kama wafanyavyo baadhi ya mastaa walio wengi.

“Ujue watu wanakuangalia wewe, sasa kama utakuwa kila sehemu wewe upo wanakuchoka, mimi nina filamu 10 tu lakini ni staa kwa kuwa najipanga.”

No comments:

Post a Comment