Tukio hilo lililopigwa chabo na shushushu wetu lilijiri wikiendi iliyopita, majira ya usiku mnene katika Hoteli ya De France iliyopo Sinza, Dar ambapo Madaha alionekana akiwa amejiachia vya kutosha kwa mwanaume huyo.
Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilizungumza na Madaha ambaye alikiri kuwa na mwanaume huyo hotelini hapo huku akidai ni meneja wake.
“Joe (Kariuki) ni meneja wangu wa Kampuni ya Candy n’ Candy Records ya Nairobi, Kenya ndiye anayesimamia kazi zangu na tayari nimeachia ngoma moja inayo-hit ya Summer Holiday,” alijitetea Madaha.
No comments:
Post a Comment