Kuna sababu zaidi ya 100 kuwa ‘ile inayoitwa’ movie ya Diamond na Wema 
Sepetu iliyopewa jina na Diamond, ‘Temptations’ haipo na kama unaingoja,
 utaingoja hadi miguu iingie tumboni. Hakuna movie.
Diamond na Wema Sepetu walikuwa wakila bata na kufurahia kama wapenzi 
wengine wanaopendana kwa dhati. Kwa kuangalia picha tu, ni rahisi mno 
kujua penzi zito kati ya wawili hawa. Picha hizo ni ishara kuwa, Diamond
 na Wema hawajawahi kuachana na Diamond amekuwa akimcheat mpenzi wake 
Penny.
Wazungu wanasema, kama hujafanya utafiti hauna haki ya kuzungumza, hivyo
 ili kuonesha kuwa hizi si brabra tu, tumefanya utafiti kwanza.
Wema, Diamond na binamu yake Romeo wakiwa Hong Kong
Ukweli wa kwanza tulioubaini ni kuwa, Diamond na Wema Sepetu walikutana 
Hong Kong na sio Malaysia. Wema alienda huko takriban wiki tatu 
zilizopita na hivyo Diamond alimfuata baada ya kumaliza show yake ya 
Malaysia. Kwa mujibu wa msichana aitwaye Alice aliyeiambia Bongo5, 
Diamond alisafiri kutoka Kuala Lumpur, Malaysia kwenda Hong Kong 
kumfuata Wema kwa ndege ya kampuni ya Air Asia.
“Nilipanda na Diamond flight moja from KUL to HKG tena ilikua ni Air 
Asia X flight number 567 alipandia KUL-LCC Terminal nilimuona kwenye 
lounge direct nikashangaa anafanya nini huku na baada kufika HKG sijui 
hata alipotelea wapi kumbe haya yote ndo alikua akiyafuata hongera zao,”
 alisema Alice.
Huko, Diamond na Wema wamekaa wote kwenye hoteli moja na mpenzi wake 
Penny hakuwa anajua kuhusu hili hadi picha hizi zilipoanza kuenea na 
yeye ameshtuka kama walivyoshtuka wengine.
Haijajulikana picha hizo zimesambazwa na nani lakini kwa mujibu wa 
vyanzo mbalimbali, kuna uwezekano kuwa picha hizo zimesambazwa na Wema 
wenyewe kwa kusudi la kumuumiza Penny. Kuna taarifa zimeifikia Bongo5 
kuwa, Penny ameumizwa mno na picha hizo na amekuwa akilia siku nzima. 
Hata hivyo binafsi hatujaweza kuthibitisha taarifa hizo.
Jitihada za kumtafuta Penny azungumzie suala hili zimegonga mwamba kwakuwa simu yake haipokelewi.
Penny
Hivi karibu kwenye birthday ya Diamond, Penny alielezea kuwa uhusiano 
wake na Diamond ndio mgumu zaidi katika mahusiano yote aliyowahi kuwa 
nayo.
“Not the easiest relationship I’ve ever had..but its the most 
intresting! When I’m down, he would make me feel on top of the world, my
 bestfriend, my brother, my soulmate, my baby, my man. My strength, my 
joy, my love, Ohhh!!! What else do I gotta say? I love u, and its been a
 blessing to have met you, u taught me that love is just Me&You the 
rest shouldnt matter or make me loose my sleep, today I ask God to bless
 u a million more times, the sweetest boyfriend ever!!! Crazie 
too..unpredictable mind, through the ups and downs Im gona hold you down
 til God says so..you have taught me that love conquers all, that Love 
is pain, but the pain is worth the while..I love you baby,” aliandika 
Penny.
Miaka ya nyuma, Wema na Penny walikuwa marafiki wakubwa lakini kwa 
mujibu wao wenyewe, urafiki wao uliharibika hata kabla ya wote 
kufahamiana na Diamond.
“Urafiki hatuna,” Penny aliliambia jarida la Mzuka kwenye makala ambayo 
haikuwa kutoka. “Mimi sidhani kama nina uadui naye personally, sijui 
yeye na urafiki hatuna. Let me just say kwamba sio kwasababu ya Diamond.
 Nadhani mimi na yeye tulikuwa tuna issue zetu nyuma ambazo hazikuwa 
resolved so tulikuwa tuna distance mimi na yeye. Tulikuwa hatuongei 
maybe kwa mwaka labda kama sio miezi nane, we had our own issues kwahiyo
 hatukuwa marafiki vile tena kama tulivyokuwa zamani. So mimi kuwa na 
uadui naye sidhani kama nina uadui. Mimi am happy unajua, mimi ndo hivyo
 mimi naishi maisha yangu am happy na nilichonacho am happy with my man,
 am happy na watu wangu so am good mimi sina tatizo naye kabisa.”
Naye Wema kwenye interview na Mzuka aliwahi kuzungumzia alivyojiskia Diamond kuwa na uhusiano na Penny, rafiki yake wa zamani.
“It’s a free world, kila mmoja ana uhuru wake wa kuishi anavyotaka yeye.
 They met, they fall in love wameanza mapenzi, mtu yoyote anaweza kufall
 in love na mtu yeyote asiwe questioned. Love doesn’t ask why, haiulizi 
kwanini, because alikuwa rafiki yangu then I can’t NO. Wapendana, I wish
 them all the best. Mimi na Penny si kwamba hatuongei sio sababu ya hii 
issue, tuna drama zetu tu za huko nyuma kwahiyo hii issue ni muendelezo 
tu,” alisema.
Ikumbukwe kuwa, Wema na Diamond waliwahi kuingia kwenye ‘kile 
kilichoonekana’ kama ugomvi mzito, baada ya Diamond kumrekodi mpenzi 
wake huyo wa zamani alipompigia na kuisambaza sauti kwenye vyombo vya 
habari.
“Sikuwahi kudhani kwamba Naseeb ni mtu wa aina hiyo kufanya kitu 
alichokifanya. Though nimesema kwamba nitaacha kama ilivyo na 
nisingependa kuiongolea lakini nilikuwa very disappointed, very very 
disappointed,” Wema aliliambia Mzuka.
Tunasubiria kushuhudia muendelezo wa drama hii kutoka kwa Malkia na Mfalme wa drama Tanzania.
SOURCE:BONGO5.COM 

 
No comments:
Post a Comment