Jana (November 21) B’Hitz Music Group iliweka wazi uamuzi wa
kuwaondoa kwenye label hiyo wasanii watatu ambao ni Vanessa Mdee,
Mabeste na Gosby.
Japokuwa Vanessa na Mabeste walitangaza wiki hii kujitoa kwenye label
hiyo, huku Gosby akiwa bado hajasema chochote, timu ya BHits imesema
kuwa wasanii hao waliondolewa kwenye label hiyo miezi miwili iliyopita
japokuwa hawaamua kutangaza.
Mabeste aliiambia Times fm kuwa ameamua kujiondoa katika label hiyo
kwa kuwa muziki wake ulikuwa haumlipi na kwamba maisha aliyokuwa anaishi
ndiyo yaliyopelekea yeye kudhaniwa kuwa anafanya show za nje, na kwamba
amechoka kuwa mzigo kwao.
Tovuti ya Times fm ilimtafuta Amani Joachim ambaye ni mwana sheria na
Chief Operations Officer wa B’Hits Music Group ili kufahamu kuhusu
sababu alizozitoa Mabeste kwa upande wa B’Hits, na mikataba ikoje na
kama watachukua hatua zozote za kisheria.
“Hiyo statement ambayo Mabeste ameamua kuisema kwangu mimi naona
haiko sawa kabisa. Sisi ni ndugu na tulikuwa tunaishi hivyo, tatizo la
mtu mmoja ni tatizo la mtu mwingine yaani tunakuwa pamoja kabisa. Na
kuna vitu vingi ambavyo Mabeste anajua kwamba tunavifumbia macho. Hata
hiyo mikataba, sisi na Mabeste kuna kipindi tume-deal hata bila mikataba
na mambo yakawa safi tu kwa sababu kuna ile heshima na kuaminiana.”
Amesema Amani.
Ameyaelezea pia madai ya Mabeste kuwa mabadiliko yake katika maisha
ndiyo yaliyosababisha B’Hits kuhisi kwamba anapiga shows za nje.
“Mabeste inabidi aangalie statements zake, na muda ambao anaamua
kutoa hizo kauli kwa sababu kati yetu sisi tuna siri nyingi sana
(Mabeste na Upande wa B’Hits). Tusifike sehemu kwamba tukaanza
kufaidisha kila mtu, hicho ndicho kitu ambacho ningependa kukiweka sawa.
Hizo shows na vitu vingine ambavyo labda alikuwa anavifanya akiwa nje
tunavifahamu vingi tu, lakini kutokana na ule u-brother na nini
tunavichunia tu.” Ameeleza kiongozi huyo wa B Hits.
Hata hivyo Amani amekubaliana na kuwepo kwa ubovu wa soko la muziki
ambapo amesema hata shows zikiwepo bado malipo yanayotolewa yako chini
kiasi kwamba Kampuni haliwezi kuendeshwa kwa kutegemea kugawana kipato
hicho na msanii.
Aliongelea pia madai ya Mabeste kuwa B’Hits haikuwa inamfanya atengeneze pesa kupitia muziki wake.
“Well, hopefully kule anakoenda atapata. Tunaelewa Mabeste ana
majukumu, maisha yake tunajua kwamba yamebadilika kwa namna flani.
Personally nafahamu, sijui akina Harmy na Pancho. That’s why I’m ready
to stay quiet kwenye vitu kama hivyo, nilikuwa tayari kukaa kimya…sina
haja ya kufunguka ni vitu vingapi ambavyo Mabeste ameshafanyiwa katika
hali ya u-brother, I will not say them kwa sababu kipindi mimi navifanya
nilivifanya katika good will na nilitaka iishie hivyo, Amani will never
say them.”
C.E.O wa B'Hits Hermy B aliuambia mtandao wa Bongo5 kuwa Vanessa,
Gosby na Mabeste hawana shukurani kwa kile ambacho B Hits imewafanyia na
kutoa mfano kuwa alitoa shilingi million nane mfukoni kulipia video ya
Closer ya Vanessa na kiasi kingine kulipia kazi alizofanya nje ya
studio za B Hits, fedha ambazo hazijawahi kurudi.
Nae Amani Joachim alitoa ushauri kwa Vanessa, Mabeste na Gosby kwa
ujumla kuwa wawe na amani na waendelee kufanya mambo yao na kuacha
kutengeneza vita kati yao na B’Hits kupitia media kwa kuwa hata yeye
ameamua kuyafumbia macho mengi.
Lakini vipi kuhusu hasara ambayo B’Hits itaipata kutokana na kuondoka
kwa wasanii hao kwa kuwa walichukuliwa wakiwa hawana majina na wakati
huu wanaondoka wakati wameanza kuwa productive.
Mwana sheria na Chief Operations Officer wa B’Hits anaeleza.
“They were real productive na naweza kukwambia kweli hawa watu wako
very talented, na B’Hits haijawahi kum-house mtu ambaye ni mbovu, na ndo
maana watu wanashangaa kwa nini mna nyumba kubwa ya media halafu mna
watu watatu tu, sisi kuna kipindi tulikuwa na msanii mmoja tu Mabeste
for like 4 years, ni kwa sababu tunaangalia talent.
“Na kusema kwamba sasa hivi tutakuwa hatujarudi nyuma utakuwa ni
uongo, kuondoka kwao ndio tutarudi nyuma steps kadhaa, lakini pia
kutokana kwamba plans tulizopanga kufanya wakati tukiwa nao zilikuwa
hazijafika kuiva, we are ready to do that with someone else, Mungu
hajagawa kipaji kwa watu wawili au watatu.”
Amesema anaamini baada ya Gosby, Vanessa, na Mabeste watakuja watu wengine ambao wana vipaji pia.
Kauli ambayo inaungana na ile ya Hermy B kuwa B’Hits itatangaza wasanii wapya wa label hiyo mwanzoni mwa mwaka ujao.
Tovuti ya Times fm ilitaka kufahamu kutoka kwa mwana sheria huyo
kuhusu mkataba kati ya B’Hitz na wasanii hao na damages/athari za
kuvunja mkataba huo zikoje na iwapo watawadai wasanii hao.
Amesema mikataba ilikuwa tight lakini kwa mazingira ya Tanzania na
hali halisi ya kipato cha wasanii wa Tanzania hiyo mikataba inakuwa kama
useless kwa kuwa kiasi kinachotakiwa kulipwa na msanii huyo ni kikubwa
kuliko hali halisi ya maisha ya msanii husika.
“Ukimchukua bwana mti ukampeleka mahakamani, mahakama inaangalia
damage ambayo imeingia katika kampuni, na mwisho wa siku inachukua
maamuzi ambapo itakwambia bwana mti kama amepatikana na kosa amlipe
bwana jose million 150 Kwa mfano, haimfungi. Problem ni kwamba bwana mti
hana hata shilling 200 mfukoni mwake, we unadhani utamfanyaje bwana
mti?” Alieleza kwa mfano.
“Kwa sababu mahakama ikishakupa judgement inakuacha ukatafute hiyo
hela, haimfungi mtu. Kesi za madai sio kesi za jinai..sasa hapo imagine
hapo ni wasanii wangapi leo unawafanyia kazi ya million 40 Million 50,
ambayo ukiingia katika intellectual property court (mahakama ya maswala
ya copy right), na copy right ni very expensive, tunaongelea six
figures, eight figures. Sasa angalia ni wasanii wangapi hapa Tanzania
wanaweza kukulipa eight figures.?” Amesema.
Kutokana na hali hiyo amesisitiza kuwa kuna haja ya kuwalipa wasanii
pesa nyingi katika kazi zao huko wanakoenda kufanya ili wanapopata
matatizo waweze kulipa, na kwamba bila hivyo mikataba ya label na
wasanii Tanzania itakuwa useless.
Hii inamaanisha kuwa hakuna hatua zozote za kisheria ambazo B’hits itachukua kudai fidia kutoka kwa wasanii hao.
Hata hivyo uongozi wa B’Hits umesema utaachia nyimbo nyingine za
wasanii hao zilizoko studio na kwamba zitachezwa redioni, lakini wasanii
hao hawatakuwa na haki ya kuzitumia kwa kuwa ni mali halali ya kampuni
hiyo.
Msikilize hapa Amani Joachim:
No comments:
Post a Comment