GWIJI wamuziki wa dansi, Muhidin Maalim Gurumo ameugua ghafla mapema leo na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Gurumo, Juma Mbizo na Said
Mdoe, waliokuwepo Muhimbili, wameuambia mtandao huu kuwa mwimbaji huyo
mkongwe alipatwa na tatizo la shinikizo la damu na hali ikawa mbaya
kabla ya kukimbizwa hospitalini hapo.
Wamesema kwa sasa haliyake inaendelea vizuri na amelazwa katika wodi ya Mwaisela namba 1.
Wajumbe hao wamesema siku chache zilizopita, Gurumo alikuwa kwenye afya
njema na hata siku ya Jumanne alihudhuria kikao cha kamati hiyo kilicho
fanyika Vijana Social Hall Kinondoni.
Aidha, wajumbe hao wamedai kuwa kwamujibu wa mke wa Gurumo, Bi Pili, ni
kwamba hata jana amwimbaji huyo alikuwa hana tatizo lolote na alifanya
mizunguko yake bila ya mikwaruzo yoyote.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha la Gurumo, Bi Asha Baraka
amewataka wapenzi wa muziki kuwa watulivu kwa vile hali ya mwanamuziki
huyo aliyeitumikia fani kwa miaka 53, inaendelea vizuri.
Tamasha la Gurumo limepangwa kufanyika tarehe 14 mwezi ujao katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe.
Tumuombee dua mzee wetu Gurumo.
GPL
No comments:
Post a Comment