Katika
kuelekea ufunguzi wa mgahawa wao magwiji wa soka wa klabu ya Manchester
United Ryan Giggs na Gary Neville jana waliingia kwenye mashindano ya
kupika misosi.
Giggs
na Neville kwa pamoja jana walishiriki kwenye mashindano hayo
yaliyofanyika maeneo ya Westfield Stratford City shopping centre jijini
London ikiwa ni moja ya shamrashamra ya ufunguzi wa mgawaha wao wa Cafe
Football.
Wawili hao walishindana na mpishi mkuu wa mgahawa huo, Brendan Fyldes pamoja na mpishi wa Michelin chef Michael Wignall.
Giggs
na mwenzie walipika vyakula vikuu vitatu ambavyo vitakavyokuwa
vikipatikana hapo vikiwemo Nev's Noodle Pot, Wignall's Halftime Orange
na Chocolate Pistachio Turf.
Neville
alisema: 'Shindano hili lilikuwa nafasi nzuri kwa wanunuzi Westfield
Stratford City kuona nini tumewaandalia kwenye Cafe Football.
'Mapishi matatu tuliyopika ni mfano tu uzuri wa vyakula ambavyo vitakuwa vikipatikana Cafe Football.
Mgahawa huo utafunguliwa rasmi mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment