UKAMILIFU wa binadamu ni pale anapozikwa, kabla ya hapo si kamili! 
Jumanne Rashid (24), Jumatatu iliyopita aliamka nyumbani kwake, Manzese 
Dar akiwa mzima wa afya na kuelekea kazini Kiwanda cha Urafiki Plastic 
Co. Ltd kilichopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Lakini ghafla, ukamilifu wake uliyeyuka baada ya mashine moja ya kiwanda hicho kumkata mkono wote wa kushoto na kuanguka.
Aidha, aliulalamikia uongozi huo kwamba waliuchukua mkono wake bila kuwashirikisha ndugu zake, wakauzika kienyeji jirani na kiwanda chao, tena bila kumfahamisha yeye mwenye mkono.
Aidha, aliulalamikia uongozi huo kwamba waliuchukua mkono wake bila kuwashirikisha ndugu zake, wakauzika kienyeji jirani na kiwanda chao, tena bila kumfahamisha yeye mwenye mkono.
Jumatano iliyopita, raia waliuona mkono huo na kulazimika kuwaita 
Polisi wa Kituo cha Urafiki-Ubungo, Dar  ambao  walipofika, majirani 
waliwatuhumu Wachina hao ambao ni mabosi wa Jumanne, kuhusika na tukio 
hilo kwani walikuwa na taarifa za kijana huyo kukatika mkono.

Baada ya kuufukua mkono huo, polisi walikwenda kumkamata mwekezaji 
anayemiliki kiwanda hicho cha kutengeneza mifuko ya plastiki aitwaye Lee
 Slimy na kumhusisha na tukio hilo.
Jumatano iliyopita,  lilipompata Jumanne katika wadi 
na. 12 katika Jengo la Kibasila, Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar
 es Salaam aliongeza zaidi:
“Siku ya tukio niliingia kazini kama kawaida na kuendelea na majukumu
 yangu, baadaye nikabaini tatizo katika moja ya mashine za kiwanda 
ambayo ilikuwa imezimwa kutokana na kukatika kwa umeme.
“
“
Nikaingiza mkono wa kushoto ndani ya mashine hiyo ili kurekebisha 
tatizo, lakini ghafla nikashtuka kuona umeme umewaka na mfanyakazi 
mwenzangu mmoja (hakumtaja) akawasha ile mashine na kilisababisha mkono 
wangu kukatika hapo hapo.”
Jumanne alisema baada ya tukio hilo alikimbizwa Hospitali ya Palestina, Sinza, Dar kabla ya kuhamishiwa Muhimbili.
“Iliniuma sana, niliuacha mkono wangu ndani ya mashine nikawa sijui ulipo. Hakuna bosi aliyekuja kuchangia gharama za matibabu. Nashangaa kusikia leo (Jumatano iliyopita) mkono wangu umeonekana ukiwa umezikwa,” alisema kwa masikitiko Jumanne mkazi wa Manzese, Dar.
juzi tulimtafuta kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Komba ili azungumzie suala hilo lakini bila mafanikio.

No comments:
Post a Comment