
UKIFIKA katika mtaa anaoishi mwanamuziki Diamond maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es Salaam utaanza kuhisi kuwa kuna staa anayeishi maeneo hayo, macho ya wengi huanza kumtazama mtu anayeelekea katika geti la nyumba anayoishi msanii huyo. (HM)
Muda wote geti hilo limefungwa. Ili uweze kuingia ndani itakulazimu 
ubonyeze kengele itakayoashiria kuwa kuna mgeni nje anahitaji kuingia 
ndani. Hata hivyo hauwezi kupenya kirahisi ndani hadi uulizwe shida yako
 na kama hauna miadi na mtu yeyote anayeishi ndani ya nyumba hiyo 
haitakuwa rahisi kuingia.
na kushuhudia ukimya wa hali ya juu ilhali kuna watu ndani. Baada ya 
kufunguliwa geti tuliingia ndani na kupokewa na Diamond aliyekuwa 
ameketi katika sebule iliyonakshiwa na mapambo makini ukutani huku ikiwa
 na samani chache lakini za gharama kubwa.
Tulitumia saa mbili mfululizo katika mahojiano na Diamond ambaye 
alifunguka kwa kila swali aliloulizwa na kujibu kwa ufasaha na ufafanuzi
 mpana.
Mwanaspoti: Utendaji kazi wako ukoje katika muziki?
Diamond: Nina mipango makini katika kazi zangu. Mambo yote lazima
 yapitie kwa meneja wangu ndipo yanifikie mimi, mara nyingi mtu hawezi 
kuzungumza na mimi moja kwa moja lazima apite huko na hiyo ndiyo staili 
ya Diamond. Nimejipanga kuhakikisha nafanya kazi gani, kwa wakati gani 
na sikurupuki tu, japo katika utengenezaji wa nyimbo zangu naweza 
nikapata wazo basi hapo hapo nikatengeneza mistari.
Mwanaspoti: Utendaji kazi wako ukoje kuanzia asubuhi hadi jioni?
Diamond: Saa tano asubuhi, nikishaamka kitu cha kwanza ni kwenda 
'gym', mara nyingi ni hapa nyumbani kama unavyoona hapo nje kuna sehemu 
ya mazoezi na sehemu
nyingine zilizopo ndani, mara nyingi hutumia muda wa saa moja. Ifikapo 
saa sita na nusu huwa naanza kufanya kazi zangu lakini itategemea na 
ratiba zangu za siku ambazo ndio mwongozo wangu wa kuimaliza siku. Baada
 ya hapo napumzika kwa muda fulani na baadaye jioni huendelea na kazi na
 mara nyingi kazi zangu huwa nazimaliza usiku wa manane.
Mwanaspoti: Unalala saa ngapi? Na unalala kwa muda gani?
Diamond: Muda wangu wa kulala mara nyingi ni saa kumi na moja 
alfajiri na kama sikuwa na kazi nyingi studio basi nitalala saa nane 
usiku. Muda wangu wa kulala ni saa sita mpaka nane kwa siku. Ila hata 
kama nikilala mapema kuamka ni saa tano asubuhi ila itategemea na nini 
ninakifanya siku inayofuata na kama nina kazi maalumu na ya mapema 
itanilazimu niamke mapema ili kuzikamilisha.
Mwanaspoti: Shughuli gani zinazokuchelewesha mara kwa mara kulala?
Diamond: Ni kurekodi na wakati mwingine shoo. Kwa wiki ninafanya 
shoo nyingi, kama ni tatu basi siku zote tatu nitalala alfajiri. Siku 
nyingine zinazosalia ninalala usiku wa manane kwa kuwa huwa nakuwa 
studio na sehemu nyingine ambazo hunilazimu kufanya kazi kwa kipindi 
kirefu usiku.
Mwanaspoti: Kati ya usiku na mchana ni muda upi unaopenda kurekodi?
Diamond: Kazi zangu narekodi usiku na ndiyo muda ninaopendelea 
zaidi. Mara nyingi napenda kurekodi saa 7 usiku ili niwe na muda na saa 
nyingine ni kuepuka lawama kurekodi mchana, kwasababu vijana wengi 
chipukizi wataona napendelewa. Unajua ninapoingia studio napenda kufanya
 kazi kwa muda mrefu, hata hivyo iliyo bora sifanyi bora liende na 
siwezi kufanya kazi na prodyuza anayenipeleka tu, ni lazima na mimi 
nipime kama kazi niliyoifanya inakwenda vile ninavyotaka au kama yeye 
anavyotaka ilimradi tufanye kazi nzuri na iliyo
bora.
Mwanaspoti: Unatumia muda gani kurekodi singo moja na kwa upande wa video ni siku ngapi?
Diamond: Inategemea, inaweza kuwa siku mbili au miezi sita lakini
 nyimbo nyingi zinatumia muda mwingi kwasababu wakati mwingine naanza 
halafu napata shoo hivyo inanibidi nipange muda mwingine wa kurekodi. 
Kuna nyimbo zangu ambazo nilizifanya kwa muda mrefu sana hizo huwa 
sizisahau ikiwemo Ukimwona, Mbagala, Nataka Kulewa na nyinginezo. 
Nakumbuka katika kazi nilizofanya kwa muda mfupi ni My Number One 
nilioufanya kwa prodyuza Sheddy Clever kwa kipindi kifupi sana pamoja na
 Mapenzi Basi sambamba na Binadamu hizi ni baadhi ya kazi ambazo 
hazikunipasua sana kichwa kuzikamilisha.
Mwanaspoti: Una prodyuza wako maalumu au studio yako mwenyewe?
Diamond: Sina prodyuza maalumu kila kazi nitakayotaka kuifanya 
ninatafuta prodyuza yule ninayemtaka hata kama sijawahi kufanya naye 
kazi. Ninafanya hivi nikiwa na malengo maalumu kwa kujiweka vizuri mimi 
kama msanii na hata kuwapa nafasi maprodyuza mbalimbali kutia mkono 
kwenye kazi ya mikono yangu. Ninaogopa kuwa na prodyuza maalumu kwa kuwa
 najua atanisumbua ikiwa atajua kwamba namtegemea yeye pekee katika kazi
 zangu. Studio sina kwa sasa ila nina mikakati ya kuwa na studio kwani 
nimeshanunua baadhi ya vifaa.
Mwanaspoti: Unadhani ndiyo sababu iliyokufanya ukagombana na Bob Junior au Manecky?
Diamond: Hapana haya mambo yalishapita lakini nilijifunza mengi 
ndiyo maana niliamua kuja na staili hii. Naogopa kubaki kuwa msanii 
ninayetegemea prodyuza fulani, bila yeye siwezi kufanya muziki, lakini 
mimi ni Diamond ninaweza kufanya muziki na prodyuza yeyote naye 
akaonyesha ufundi wake kupitia kazi yangu.
Mwanaspoti: Shoo gani kubwa kuliko zote uliyowahi kufanya ambayo haijawahi kujirudia?
Diamond: Diamond Forever. Hii ilikuwa kubwa sana ambayo sitakaa 
nikaisahau, ilihudhuriwa na watu wakubwa na maarufu hapa nchini hata 
hivyo ilikuwa ya kipekee ambayo haijafanana na yoyote ile. Ya pili ni 
ile ya Dar Live ambayo nilifanya baada ya kushuka katika helikopta ile 
pia ilikuwa kubwa. Lakini kwa nje ya nchi ni Mombasa na Comoro huko 
nilifanya shoo kubwa sana ambazo siwezi kuzisahau.
Mwanaspoti: Ni shoo ipi iliyowahi kukuingizia pesa kubwa kuliko zote?
Diamond: Shoo ile ya Mlimani City ya Diamond Forever, ile 
iliniingizia pesa kubwa sana na tangu pale ndipo nilipoanza kufurahia 
matunda ya kazi yangu. Nilifanya shoo pia Burundi, Mombasa na Congo shoo
 hizi ziliniingizia kiasi kikubwa sana cha pesa siwezi kutaja ni 
shilingi ngapi lakini ni pesa nyingi ambazo sitakaa nizisahau.
Mwanaspoti: Shoo ipi ilikuwa ya bei chee ambayo huwezi kuisahau
Diamond: Kwa kweli siwezi kusahau nilipofanya shoo yangu ya 
kwanza kubwa mwaka 2009 kwenye Fiesta iliyofanyika Dar es Salaam, 
ilikuwa ndiyo shoo yangu ya kwanza na kubwa wakati huo nilikuwa natamba 
na wimbo Kamwambie, ilinichukua muda mrefu sana kujiandaa mimi pamoja na
 madansa wangu wanne tulilipwa Sh 50,000 lakini sikukata tamaa kwani 
ilikuwa ndiyo mwanzo wangu wa kujuana na watu wengi na wadau wakubwa wa 
muziki hapa nchini ambao nilikutana nao kwenye ile shoo.
Mwanaspoti: Kwa hivi sasa ni shoo gani ambayo unaweza kusema kwamba utafanya kwa bei ya chini na ni shilingi ngapi?
Diamond: Shoo ninayoweza kufanya kwa bei ya chini kabisa ni Sh 10
 milioni za Kitanzania na hii labda nione anayeniomba nifanye shoo hiyo 
hayuko vizuri na pengine ni rafiki yangu na hawezi kuninyonya, si hivyo 
tu itategemea pia ni kampuni gani na ni watu wa aina gani ambao 
watanitaka nifanye nao kazi.
Mwanaspoti: Kwa kawaida Diamond ni msanii wa gharama gani kwa shoo moja ndani na nje ya nchi?
Diamond: Kwa kawaida shoo moja ninafanya kuanzia Sh15 milioni 
mpaka Sh20 milioni kulingana na muda nitakaofanya shoo. Pia zile za nje 
ninafanya kwa gharama ya Dola 20,000 mpaka 30,000 yaani ni Sh32 milioni 
mpaka 48 milioni hivi kwa fedha za Tanzania na nikiwa huko nahakikisha 
ninafanya kazi vile inavyotakiwa. Lakini hali ni tofauti inavyokuja shoo
 ile ya uwanjani yaani hapa nazungumzia shoo kubwa zinazofanyika nje ya 
ukumbi, hizi natoza Dola 20,000 ambayo ni sawa na Sh32 milioni 32 kwa 
fedha ya Kitanzania.
Mwanaspoti: Kuhusu madansa wako unawachukuliaje?
Diamond: Ni kama kaka zangu na ninawapenda sana kwani tumetoka 
nao mbali na wanajua kuwa tunafanya kazi pamoja kutengeneza maisha hivyo
 ni kama ndugu zangu na tunasaidiana kwenye kila jambo ukizingatia kuwa 
kile tunachokipata tunagawana. Kwa kweli najitahidi sana kuwaambia hasa 
kuhusiana na masuala ya kimaisha, nahusika katika maisha yao ya kila 
siku na nijuavyo mimi nikikosea tu mmoja akapotea kundi langu litakuwa 
limeharibikiwa maana kila mtu namtegemea kwa upande wake. Kwa sasa 
wamejenga nyumba zao na wanaendelea vizuri kimaisha hilo ndilo sharti 
langu lazima wafanye mambo ya maendeleo kwa kile tunachokipata.
Mwanaspoti: Umesafiri nao nchi ngapi, na kwanini unapenda kuambatana nao?
Diamond: Nimesafiri nao sehemu mbalimbali kama Burundi, Comorro 
na sehemu nyinginezo ambako nimekwenda kufanya shoo, sina tabia ya 
kusafiri peke yangu hata nikienda Ulaya na hata Marekani lazima niwe 
nao. Ninapenda kuwa nao kwani ni sehemu ya muziki wangu na imefika 
wakati nimekuwa nataka mapromota kuhakikisha wanatulipia mimi na madansa
 wangu kwa ajili ya shoo hasa tutakapojua kuwa shoo fulani itaingiza 
watu wengi au udhamini mkubwa.
Mwanaspoti: Kuna safari ambayo umewahi kusafiri peke yako?
Diamond: Ziko nyingi, nilienda mwenyewe kutokana na ukubwa wa 
shoo, lakini ni miaka kadhaa nyuma, baadaye nilijiwekea mikakati kwamba 
siwezi kusafiri mwenyewe wakati shoo nahitaji kufanya na madansa wangu, 
awali mapromota walikuwa wagumu kunielewa na wapo waliokataa. Niliachana
 nao na kuwataka wakishajipanga na kuhakikisha kwamba wanaweza 
kunichukua mimi na madansa wangu watafanya hivyo.
Mwanaspoti: Umewahi kuwatema madansa?
Diamond: Sijawahi kubadilisha madansa kwa sababu wanajua kazi 
yao. Ingawa nilikuwa na madansa sita nilipokuwa naanza muziki lakini 
niliachana na wawili kutokana na utendaji wao wa kazi. Wawili hawa 
hawakuwa wabunifu kila siku walikuwa na staili ileile, niliamua kuchagua
 vichwa ambavyo vikikaa na mimi mwishowe tunatoka na kitu makini na 
chenye kueleweka. Kulikuwa na tatizo pia la kukosea stepu wakati wa shoo
 hili lilikuwa likinishushia sana hadhi yangu jukwaani, hapo ndipo 
nilipoamua kuwaondoa.
Mwanaspoti: Kwa upande wa malipo unawalipaje?
Diamond: Ninawalipa vizuri lakini siwezi kutaja kiwango ila 
ingekuwa kwangu ningetaja, hiyo ni haki yao wao wenyewe kutamka ila mimi
 siwezi kutaja. Malipo ninayowalipa yapo machoni mwa watu 
wanaowazunguka, dansa kujenga nyumba kumiliki baadhi ya biashara si 
jambo dogo, hivyo ninawalipa vizuri. Na hata gharama za kusafiri ndani 
na nje ya nchi vyote ni juu yangu, malipo tunayoyapata tunagawana.
Mwanaspoti: Unakumbana na changamoto zipi katika kazi yako?
Diamond: Nakumbana na mengi, kwanza unapokuwa msanii unayeongoza 
lazima upate vikwazo vingi. Nakumbana na watu wengi wanaonichukia na 
kunitusi bila sababu za msingi, hata hivyo nasingiziwa vitu vingi 
ambavyo havipo nadhani hii ni changamoto iliyotokana na kufanya vizuri 
katika muziki.
Wapo ambao wanamwona Diamond anafanya vizuri kwenye muziki badala ya 
kukaa na kuangalia nimepita wapi na wapi anaanza kutoa lawama kwamba 
ameibiwa na mengine ambayo kimsingi hayana maana.
Mwanaspoti: Siku za hivi karibuni kuna maprodyuza na wasanii 
wasiofahamika ambao walijaribu kutengeneza kazi yako ya My Number One na
 kukutusi kupitia wimbo huo na wapo waliotunga mashairi mengine 
yaliyozungumzia maisha yako kabla hujawa staa, ulijisikiaje? Na 
unachukua hatua gani?
Diamond: Awali niliumia sana nilipoibiwa mashairi ya wimbo wangu 
wa Mbagala, iliniuma sana kwa muda wa wiki nzima uchungu nilioupata 
siwezi kuuelezea. Lakini baadaye nilikomaa, huwezi amini niliposikia 
zile nyimbo nilicheka sana kisha nikawadharau sana watu waliofanya hivyo
 maana nipo kwenye hii tasnia siwezi kuchukia watu wasiojua walitendalo 
kwani na wao wapo katika kujitafutia riziki. Lakini hata hivyo sheria ya
 muziki bado haijawa makini hapa nchini
nitachukua hatua gani mwisho wa siku nitaacha kufanya mambo yangu ya 
msingi na kushughulikia wezi wa kazi zangu ambao hata hivyo hawatabanwa 
kwa lile walilolifanya.
Mwanaspoti: Msanii yupi hapa Tanzania anakutisha kama hayupo vipi huko nje ya nchi?
Diamond: Kwa hapa Tanzania sijaona mwanamuziki anayenitisha, ila 
siwezi kujua mashabiki wao ndio majaji, nafikiri kila mtu anaweza kuwa 
na mtazamo wake. Kati ya wanamuziki ninaowahusudu mimi kwa nje ya nchi 
hasa Afrika ni P Square pekee, hawa wapo katika nafasi kubwa sana kwenye
 ubongo wangu na nafikiria ni lini ninaweza kuwafikia, hiyo ndiyo ndoto 
yangu daima.
Mwanaspoti: Unapokuwa juu ya jukwaa unakumbana na vishawishi vipi ukiwa kama msanii mkubwa?
Diamond: Ninapata vishawishi vingi sana ninapokuwa jukwaani. Kwa 
kweli ninashawishiwa na wakinadada, mfano kuna mwanamke mmoja ambaye 
alikuwa mmoja wa mapromota wa shoo nchini Uingereza alitaka kunibusu 
mdomoni kwa lazima, kitendo kile kilinifedhehesha sana na nilishindwa 
nifanyeje kwani nipo ugenini na jukwaani ilikuwa ngumu sana kwangu. 
Wakati mwingine wanawake wanapanda jukwaani ili wacheze na wewe mwisho 
wa siku wanaingiza mikono kwenye suruali yaani sipendezwi kabisa na 
michezo ya namna hii.
Mwanaspoti: Umewahi kuibiwa ukiwa jukwaani?
Diamond: Nimeshaibiwa sana hasa katika hizi shoo ndogo ndogo mara
 nyingi watu wanapanda jukwaani na kuondoka na kitu chako. Nakumbuka 
nimeshawahi kuibiwa saa, pete ya dhahabu na kuna mmoja alitoa kali ya 
mwaka yaani yeye alinivua nguo kwa lazima.
Mwanaspoti: Inakuwaje nje ya muziki, unakumbana na changamoto zipi?
Diamond: Kitu ambacho ni changamoto kubwa sana kwangu ni simu 
yangu ya mkononi. Kila baada ya miezi sita au mitatu nalazimika kubadili
 namba yangu ya simu, nasumbuliwa sana na watu ambao hata hivyo hawana 
la msingi la kuniambia. Ni kweli kwamba mawasiliano ni kitu cha msingi 
na 
ninawapenda mashabiki wangu lakini namba yangu inasambaa kwa kasi ya 
ajabu kiasi kwamba nashindwa kupokea simu za maana kwa kudhani kwamba na
 hao nao ni wasumbufu.
Mwanaspoti: Ina maana milio yote ya simu hapo ni watu wanakupigia?
Diamond: Yap, unavyoona inalia kila dakika watu wanapiga hapa. 
Muda mwingi hii simu ninaweka 'silent' yaani haitoi mlio wowote kwani 
inaita kila dakika.
Mwanaspoti: Tuzungumzie uhusiano wako. Mpenzi wako wa kwanza unamkumbuka? na je uliwahi kumpa shilingi ngapi?
Diamond: Mpenzi wangu wa kwanza kabisa enzi hizo ninajifunza 
mambo haya sikumbuki vyema jina ila alikuwa anaishi Tandale na mimi pia 
nilikuwa naishi huko na mama yangu. Sikumbuki kama nimewahi kumhonga 
maana enzi hizo mimi nilikuwa napewa tu na mama yangu pesa, sikuwa na 
hela yoyote ya kumpa na ilikuwa ni kwa kipindi kifupi kama miezi minne 
hivi, hata hivyo tulikuwa tunaibana tu kwa siri nilikuwa mdogo.
Mwanaspoti: Kwanini mliachana?
Diamond: Kwanza nilikuwa sijajua mapenzi ni nini. Hata hivyo 
haikuwa rasmi na wala nilikuwa sijawa na akili ya kupenda sana na 
nilikuwa na fikra kwamba ni mchezo tu hivyo tuliachana mapema kwani hata
 yeye akili yake ilikuwa haijakomaa.
Mwanaspoti: Mpenzi wako uliyekuwa naye kabla ya kuwa staa nasikia uliachana naye baada ya kutoka kimuziki kwa nini?
Diamond: Nilimpenda sana lakini aliniacha kabla ya kutoka. Mpenzi
 wangu wa kwanza alikuwa anaitwa Sarah Sadick, sijawahi kumuhonga na 
ndiye mwanamke niliyewahi kumpenda sana. Wakati huo Naseeb Abdul kabla 
sijawa Diamond nilikuwa nahaha kuhangaika ni vipi nitatoka kimuziki. 
Msichana huyu ndiye aliyenipa hasira za kufanya muziki kwa bidii zote 
baada ya kunitema na kuanza kuhangaika na wengine na aliniita majina 
mengi yasiyo mazuri, kisa sina fedha. Si kwamba nilimuacha bali yeye 
ndiye aliyeniacha kama zali baada ya wiki kadhaa nikatoka na wimbo 
Kamwambie, taratibu nikaanza kuwa staa naye akaanza kurudi ila 
nilishamuondoa moyoni mwangu.
Mwanaspoti: Kwa nini mliachana? Unadhani hakukufaa tena kwa kuwa ulishakuwa staa?
Diamond: Alinisumbua sana kutokana na ugumu wa maisha niliokua 
nao kwa kipindi cha nyuma hadi kufikia 2009. Nilimpenda sana huwezi 
amini nilikuwa silali usingizi kwa ajili yake. Nahisi ilitokana na mimi 
kukosa kazi ndiyo maana ilifikia hatua alinipotezea. Lakini baada ya 
kupata na kujulikana alinifuata lakini sikutaka tena hata baada ya 
kuniomba msamaha.
Mwanaspoti: Umewahi kuwa na wanawake wangapi tangu uwe staa?
Diamond: Sikumbuki kwa kweli wapo wengi mno, si unajua tena wapo 
walionitaka na kunilazimisha nifanye hivyo, lakini idadi kamili siwezi 
kukumbuka na kila siku nasumbuliwa na hawa wanawake.
Mwanaspoti: Ni wapenzi wangapi ambao umekuwa nao kipindi kirefu na kuwapenda kama wapenzi wako?
Diamond: Nimewahi kuwa na wapenzi wanne katika kipindi chote cha 
ustaa wangu na sikupenda kubadili ovyo ila wengi wao hawakuweza kutimiza
 haja ya moyo wangu.
Mwanaspoti: Unaweza kuwataja majina?
Diamond: Ndiyo ila wawili wanafahamika zaidi. Wa kwanza kabisa 
alikuwa anaitwa Sarah na wa pili alikuwa anaitwa Hawa yule msichana 
niliyeimba naye katika wimbo 'Nitarejea', huyu alizidiwa ujanja na Wema 
Sepetu ambaye naye alikuja kuondoka kwangu na baadaye nikawa na Penieli 
Mungilwa.
Mwanaspoti: Mwanamke yupi unahisi ulimpenda kuliko wote?
Diamond: Mwanamke wangu wa kwanza Sarah Sadick huyu aliniingia 
sana moyoni sijajua ni kwanini. Lakini nahisi huenda kwa kuwa awali 
alinipenda kweli kwa kuwa wakati huo sikuwa na kitu. Hata hivyo nahisi 
ilitokana na mimi kutokuwa bize na wakati huo sikufikiria lolote zaidi 
ya yeye ilitokana na kutokuwa na kazi ya kufanya. Siku hizi sina mapenzi
 ya kivilee, nawaza zaidi pesa na ninaihangaikia na zaidi ni muziki 
wangu, hili ndilo la kwanza kabisa linalonifanya niwe bize mapenzi 
baadaye.
Mwanaspoti: Umeshawahi kutongozwa na wanawake?
Diamond: Ndiyo, wengi sana tena kuna mmoja kati ya wanawake 
niliowahi kuwa nao alinitongoza yeye mwenyewe ndipo nikawa naye na 
nilikaa naye katika uhusiano kwa kipindi kirefu tu. Wanaweza kumfikiria 
mwanamke fulani lakini huwezi amini ukweli ninao mimi mwenyewe na katu 
hawawezi hata kumhisi. Ninatongozwa sana kwenye mitandao ya kijamii, 
facebook, whatsapp, Instagram na kwingineko na wapo wasichana ambao 
wanatafuta namba zangu za simu na kuanza kunisumbua.
Mwanaspoti: Unapata usumbufu wowote toka kwa wanawake?
Diamond: Ndiyo, wengi sana tena kuna mmoja kati ya wanawake 
niliowahi kuwa nao alinitongoza yeye mwenyewe ndipo nikawa naye na 
nilikaa naye katika uhusiano kwa kipindi kirefu tu. Wanaweza kumfikiria 
mwanamke fulani lakini huwezi amini ukweli ninao mimi mwenyewe na katu 
hawawezi hata kumhisi. Ninatongozwa sana kwenye mitandao ya kijamii, 
facebook, whatsapp, Instagram na kwingineko na wapo wasichana ambao 
wanatafuta namba zangu za simu na kuanza kunisumbua.
Mwanaspoti: Ni mwanamke wa aina gani unataka awe mkeo?
Diamond: Kwanza ninahitaji aijue kazi yangu na ajue kwamba mimi 
ni mtu maarufu hivyo akubaliane na changamoto mbalimbali atakazokumbana 
nazo kwa kipindi atakachokuwa ndani ya ndoa, siyo siku mbili anafungasha
 virago. Pia ajue kwamba nitamsikiliza mama yangu kwanza kabla ya yeye 
hilo naliweka wazi, yeye ana nafasi yake katika maisha yangu lakini mama
 yangu nimempa kipaumbele, tatu awe tayari kuishi na mama yangu. Nne awe
 na akili na mwenye utambuzi na atakayeniongoza katika kazi zangu, 
sihitaji. Itaendelea… 
Chanzo: mwanaspoti
 
 
No comments:
Post a Comment