Aliyekuwa mbunge wa Songea mjini, Abdulrabi Ali Yusuph(66) akizungumzia
 maisha yake baada ya kufungwa jela akiwa nyumbani kwake hivi karibuni. 
Picha na Lauden Mwambona. .  
Aliyekuwa Mbunge wa Songea mjini kuanzia Oktoba 1985 hadi Aprili
 1988 alipofungwa jela miaka 11, Abdulrabi Ali Yusuph (66), amesema 
tangu atoke gerezani hadi sasa anaomba aonane na Rais Mstaafu Ali Hassan
 Mwinyi ama Rais Benjamin Mkapa na hata Rais Jakaya Kikwete lakini 
hajafanikiwa hadi leo.
                
              
Amesema aliomba nafasi ya kumwona Rais Mwinyi 
akiwa madarakani ili amweleze ya moyoni, lakini hakufanikiwa na 
aliendelea kuomba amwone Rais Mkapa hakufanikiwa na sasa anaomba amwone 
Rais Kikwete bado hajajaaliwa.
                
              
Alisema hayo katika mahojiano maalumu 
yaliyofanyika nyumbani kwake Mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea ambako 
anaishi akiwa kwenye nyumba chakavu ya urithi na wake zake wawili pamoja
 na watoto kadhaa.
                
              
Mahojiano ya mwandishi na mbunge huyo yalianza hivi. 
                
              
Mwandishi: Mheshimiwa habari za 
siku nyingi. Nimefika hapa kwa niaba ya jarida la Ndani ya Habari 
linalochapishwa na gazeti la Mwananchi, lengo hasa ni kukujulia hali. 
Watu wangependa kujua unaendeleaje hasa baada ya kifungo chako. 
Ningependa kupata maelezo yako juu ya masuala ya maisha ya gerezani na 
ya sasa ukiwa huru.
                
              
Mbunge. Kwanza kabla ya yote. Wewe upo hapa ili uuze gazeti na upate fedha. Je, mimi unanieleza vipi kuhusu mapato hayo.
                
              
 Mwandishi: Kazi ya mwandishi 
siyo biashara, bali ni  ya kijamii. Kazi ya mwandishi ni kuelimisha, 
kufundisha, kuibua kero na kutaarifu jamii. Kazi ya mwandishi inaweza 
kukusaidia ama kukuharibia kwa kuibua mambo ambayo unaweza kufanya kwa 
kuvunja sheria na kuitisha jamii.
                
              
Mbunge: Kwa maneno yako haya ni kwamba mimi sina lolote la kufaidika leo?
                
              
Mwandishi: Ni kweli sikuja hapa 
kibiashara bali kukusalimu na kupata hisia zako ama kauli yako baada ya 
kufungwa jela kwa miaka 11  ukiwa mbunge na sasa upo nje, hivyo 
tunapenda kujua uliishi vipi jela na jamii inakuonaje baada ya kutoka?
                
              
Mbunge:Basi kwa kuwa umefika 
hapa, nitasema machache, lakini kama utakuja baada ya kujipanga, 
nitaeleza mengi  mno. Mimi ninazo kero na mambo mengi baada ya kuishi 
gerezani na kwa kweli nina masikitiko mengi ambayo yananisononesha sana.
                
              
Mwandishi:Nashukuru Mheshimiwa, naomba udokeze hisia zako walau kidogo.
                
              Mbunge: Kwanza  ninayo masikitiko
 mpaka leo kwa viongozi wakuu wa taifa hili. Nasikitika mpaka leo kwa 
kunyimwa nafasi ya kuonana na walau mmoja kuanzia Rais wa  awamu ya 
pili, Ali Hassan Mwinyi, awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na hata awamu ya 
nne Jakaya Kikwete
  -MWANANCHI
 
 
No comments:
Post a Comment