Tunafanya kazi usiku na mchana, tunahangaika huku na huko lakini mwishowe tunafikiria jinsi ya kuboresha na kufurahia maisha na wapenzi wetu na kupata utulivu na amani katika maisha ya kimapenzi.
Ndiyo maana kila mmoja anajitahidi kutafuta mwenza sahihi ambaye anaweza kumfanya asijute kuwa naye na mwishowe furaha itawale.
Lakini katika jamii yetu kuna watu ambao kutokana na ugumu wa maisha ama tamaa zao wameamua kuigeuza miili yao kuwa kitega uchumi. Wanawake hawa wako tayari kulala na mwanaume yoyote ili mradi wapewe fedha.
Kwa kifupi watu hawa wanadharauliwa na kila mmoja atashangaa kuona au kusikia mwanaume anaoa msichana aliyekuwa malaya. Hata hivyo, ukweli ni kwamba, kuna wanaume wanawaoa. Katika hili hata wewe unaweza kuwa shahidi
No comments:
Post a Comment