Ni picha ambazo zimekua zikizungumziwa kwenye mitandao ya kijamii na hata kwenye mitandao mingine ya habari nchini Tanzania zikimwonyesha mchezaji wa Yanga Mrisho Ngassa akiwa mapenzini na mwimbaji Snura wa bongofleva.
Snura anasema mwanzo wa hizi picha kusambaa ni baada ya kupoteza simu yake, namnukuu akisema ‘Millard hizo picha hazina uhusiano wowote unaounganishwa kimapenzi kati yangu na Ngassa ila ni sehemu ya vipande vya movie yangu inaitwa ‘Majanga’ ambayo nimeanza kuifanya na Ngassa amecheza ndani yake kwenye scene za mapenzi, yani Snura kwenye movie amecheza kama binti mrembo anaerukiarukia Wanaume’
‘Simu
yangu ilipotea ndio maana wamezipata hizo picha, wakati tunashoot
tulikua tunapigapiga tu hayo mapicha, mi sikuwa nataka kuzitoa kabisa
manake movie yenyewe bado naifanya nusunusu kutokana na kukosa muda, hii
ishu imeniletea sana matatizo manake mwingine anakua haamini
unachokiongea na hakuna kitu kinauma kama kuongea ukweli alafu mtu
anasema unadanganya’ – SnuraKwa kumalizia Snura anasema ‘Ngassa alinipiga muda mfupi tu baada ya picha kuanza kusambaa akauliza mbona hizi picha zinasambaa hivi Snura? nikamwambia usinielewe tofauti babaangu kwa sababu mimi mwenyewe sikutaka zitoke, picha nilizopiga nyinginyingi tu wakati tunatengeneza movie ila naona watu wameona hizi ndio nzuri kwa skendo
No comments:
Post a Comment