MNYONGE mnyongeni haki yake mpeni, skandali ya kumbaka na 
kumwambukiza Ukimwi mwanafunzi, inamtafuna na kumuumiza Mbunge wa Urambo
 Magharibi (CCM), Juma Athuman Kapuya.
Kuhusu ukweli wa skendo hiyo, vyombo vya 
sheria vitazungumza lakini gazeti Uwazii limezungumza  naye  na  hizi  ni  dondoo fupi  za  mazungumzo  yao.
Kwa mujibu wa gazeti la Uwazi, denti huyo amekuwa akijulikana kama Felista, ila anatambulika pia kama Halima Hamad, hivi karibuni aliamua kujiita Leylat na wakati mwingine Leila.
Jina
 ambalo alijitambulisha kwa  Kapuya  ni Halima Hamad, upande 
mwingine hujitambulisha kama Halima Humudi, yaani huchezea ubini.
Gazeti hilo limeripoti kuwa, mwezi mmoja kabla ya sakata la Kapuya 
halijapamba moto, Felista alizungumza na waandishi wake  wawili kwa 
nyakati tofauti, akielezea uhusiano wake na mheshimiwa huyo ambaye kwa 
sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Miundombinu.
Felista
 alimweleza mwandishi wa kwanza ambaye ni mwanamke: “Nina stori kuhusu 
Kapuya, yule ni mtu wangu, ila subiri kidogo nitakupa stori kamili.” 
Siku mbili baadaye, Felista alimfuata 
mwandishi wa pili ambaye ni wa kiume, akamwambia: “Kapuya ananitongoza, 
ngoja mambo yakae sawa nitakwambia.”
Hata hivyo, waandishi hao waliamua kumpotezea.
Hata hivyo, waandishi hao waliamua kumpotezea.
Baada ya sakata hilo kuibuka kwa nguvu, 
kasi na ari, waandishi hao walimpigia simu Felista kumuuliza ilikuwaje 
akalifikisha suala mbali zaidi, huku akijisema yeye ni mwanafunzi wakati
 siyo kweli?
Felista alimjibu mwandishi wa kwanza: “Huyo aliyepeleka 
hizo habari ni Leylat. Mimi Kapuya nafahamiana naye kwa sababu 
nilishiriki vikao vya usuluhishi kati ya Leylat na Kapuya. Walimalizana 
vizuri. Mimi kama shahidi nilipata shilingi 3,000,000.
“Siku ya kwanza nilipewa shilingi 2,300,000, baadaye alinimalizia shilingi 700,000, tukawa tumemalizana.”
Mwandishi wa pili alipomuuliza, alijibu: 
“Jamani siyo mimi, yule ni Leila. Yule mtoto sijui kafikishaje hayo 
mambo huko, ila mimi najua kila kitu.”
Historia  ya  huyu binti   kwa  mujibu  wa  gazeti  la  Uwazi:
Felista wa Kapuya ndiye yule binti 
aliyewahi kumtapeli mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma kupitia 
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama).
Msichana huyo, alidai yeye 
ni yatima, akiishi kwa tabu sana, Mama Salma akaingia mkenge na kumpa 
kiwanja Mbagala. Baadaye ilipokuja kujulikana, alishtakiwa kwa utapeli, 
akapelekwa mahabusu kwenye Gereza la Segerea, Dar es Salaam.
Felista alikiri kuwekwa Segerea kisha akajitetea: “Kuna watu walitaka kunigombanisha na Mama Salma lakini mbona nilitoka?”
Felista,
 alishawahi kumuibia marehemu Steven Kanumba kamera, alipokwenda ofisini
 kwake, akijidai ni yatima na ana kipaji cha kuigiza, alipopata mwanya 
tu, alimliza supastaa huyo ambaye alifariki dunia, Aprili 7, mwaka jana.
Ukiachana
 na hilo la Kimei ambalo limetajwa na Kapuya, yapo matukio mengine 
ambayo Felista alishayafanya, ikiwemo kudanganya anasoma alipiwe ada, 
vitabu, madaftari na sare za shule, kumbe ni ‘gia’ yake ya kupata fedha 
kwa njia ya udanganyifu.
Uchunguzi wa gazeti  hilo  unalo jawabu kuwa kama kuna uongo ambao jamii 
haipaswi kubisa kukubaliana nao ni huu kwamba Felista ana umri wa miaka 
16 na anasoma sekondari.
  
Gazeti hilo limebaini kuwa Felista ni mama wa mtoto mmoja na lilipombana alikiri: “Ni kweli nina mtoto mmoja, nina umri wa miaka 21.”
Gazeti hilo limebaini kuwa Felista ni mama wa mtoto mmoja na lilipombana alikiri: “Ni kweli nina mtoto mmoja, nina umri wa miaka 21.”
VIDEO  FUPI
 




 
No comments:
Post a Comment