Serikali yatangaza nafasi za kazi 2,748.
Serikali
 kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma 
inawatangazia watanzania  wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi 
wazi za kazi 2,748 kwa ajili ya waajiri mbalimbali Nchini.
 Kwa 
mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. 
Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya 
Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali wa Ofisi za Umma.
 Daudi alitaja nafasi za kazi zinazotangazwa kuwa ni Afisa Uvuvi daraja 
la ii, Mvuvi msaidizi daraja la ii, Afisa Mifugo msaidizi daraja la ii, 
Afisa mifugo daraja la ii, Mteknolijia wa samaki daraja la ii, Daktari 
wa mifugo daraja la ii,Afisa utafiti Mifugo daraja la ii, Daktari 
utafiti Mifugo daraja la ii, Fundi sanifu Maabara Mifugo daraja la ii, 
Mkufunzi Mifugo daraja ii, Mkufunzi wa Mifugo msaidizi na Daktari 
Mifugo.
 
 Kada nyingine ni Mkufunzi daraja la ii, Mtekinolojia wa
 Samaki msaidizi daraja la ii, uunda boti daraja ii, nafasi 2, Dereva wa
 vivuko daraja la ii, msaidizi mifugo,afisa kilimo daraja la ii, Afisa 
kilimo msaidizi daraja la ii, Mhandisi kilimo daraja la ii, Fundi sanifu
 daraja la ii, Afisa utafiti kilimo daraja la ii, Mkufunzi wa kilimo 
msaidizi, Afisa kilimo msaidizi daraja la iii,Dereva daraja la ii, 
mlinzi, Mhasibu mkuu daraja ii, Msanifu lugha mkuu iii  na Afisa vipimo.
 
 Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira nafasi hizo za kazi ni 
kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Katibu 
Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mkurugenzi Halmashauri 
Wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mlele, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpanda, 
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nkasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
 Sumbawanga na Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni.
 
 Nafasi 
nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyerwa, 
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chato, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
 Misenyi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ngara, Mkurugenzi Halmashauri
 Wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukoba, Mkurugenzi 
Halmashauri ya Mji Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkinga, 
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilindi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji 
Korogwe,  Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Pangani, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Korogwe 
na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muheza.
 
 Nafasi hizo pia ni 
kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulyankulu, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uyui, 
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nzega, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji 
Nzega, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Manispaa ya 
Tabora, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ikungi, Mkurugenzi Halmashauri 
Wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iramba, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Manyoni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Singida,
 Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Itilima na Mkurugenzi Halmashauri 
Wilaya ya Ushetu.
 
 Waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri 
Wilaya ya Msalala, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kishapu, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Bukombe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Meatu, 
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri 
Wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kahama, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Bariadi, Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga, 
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyasa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
 Namtumbo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbinga, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Manispaa ya Songea, Mkurugenzi
 Halmashauri Wilaya ya Nyang`wale, Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela, 
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Misungwi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
 ya Ukerewe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Geita na Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Magu.
 
 Nafasi hizo za kazi pia ni kwa 
aajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tandahimba, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Newala, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Masasi, 
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya 
Gairo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mvomero, Mkurugenzi Halmashauri 
Wilaya ya Kilombero, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulanga, Mkurugenzi
 Halmashauri Wilaya ya Morogoro, Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, 
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Tunduma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya 
Momba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbarali, Mkurugenzi Halmashauri 
Wilaya ya Ileje, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyela, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Chunya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbozi, 
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbeya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
 Rorya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Serengeti, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Bunda, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tarime, 
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Butiama, Mkurugenzi Halmashauri 
Manispaa ya Musoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ruangwa, Mkurugenzi
 Halmashauri Wilaya ya Nachingwea, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya 
Lindi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mwanga na Mkurugenzi Halmashauri
 Wilaya ya Hai.
 
 Katika nafasi hizo waajiri wengine ni 
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rombo, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa 
ya Moshi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kahama, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Uviza,  Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Monduli, 
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Babati, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya 
ya Hanang, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Simanjiro, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya 
Kisarawe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rufiji, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkuranga, 
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iringa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya 
ya Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Makete, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chamwino,
 Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpwapwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
 ya Kondoa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kongwa na Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Bahi, 
 
 Waajiri wengine katika nafasi hizo
 za kazi ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chemba, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kongwa, 
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilolo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya 
ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ludewa, Mkurugenzi 
Halmashauri Wilaya ya Wanging`ombe, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya  
Kigoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kigoma, Mkurugenzi Halmashauri 
Wilaya ya Kasulu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kakonko, Katibu 
Tawala Mkoa Arusha, Katibu Tawala Mkoa Pwani, Katibu Tawala Mkoa Dodoma,
 Katibu Tawala Mkoa Iringa, Katibu Tawala Mkoa Kilimanjaro, Katibu 
Tawala Mkoa Mtwara, Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Katibu Tawala Mkoa 
Ruvuma, Katibu Tawala Mkoa Tabora, Katibu Tawala Mkoa Kagera, Katibu 
Tawala Mkoa Dar es salaam, Katibu Tawala Mkoa Rukwa, Katibu Tawala Mkoa 
Katavi, Katibu Tawala Mkoa Njombe, Katibu Tawala Mkoa Njombe, Katibu 
Tawala Mkoa  Simiyu na Katibu Tawala Mkoa Geita.
 
 Daudi amesema 
mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 10 Desemba, 2013. 
Aidha amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kutambua kwamba Kila 
mwombaji kazi atapangwa katika kituo chochote cha kazi bila kujali eneo 
au mahali alipoomba kutokana na mahitaji ya mwajiri pamoja na idadi ya 
waombaji katika eneo husika.
 
 Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
 Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 27 Novemba, 2013.
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment