Kuna wakati nilikuwa navaa shanga kwenye kiuno sio kwamba nilipenda ila mpenzi wangu kipindi hicho ndio alikuwa anapenda nivae akisema anapoziona anasisimuka lakini baada ya kuachana naye nikaachana nazo kwakuwa sikuwa nazipenda kuvaa bali kumridhisha tu..
Kitu cha kushangaza ni kwamba kuna rafiki yangu anaolewa karibuni mchumba wake amemletea shanga avae, anasema yeye anapenda kumuona mpenzi wake akiwa amevaa ndipo nilipo mshauri azivae baada ya kumpa story yangu hapo juu..
Wanaume kuna raha gani ambayo mnaipata pindi wapenzi wenu wanapo vaa shanga????na je ni wanaume wa makibala fulani ama wote kwa ujumla? maana rafiki yangu huyo mchumba wake mkuria na ndicho kilicho zidi nishangaza...na mwanaume aliyenifanya mimi nivae ni mmakonde ndio inazidi kunichanganya..
Sio vibaya nikufahamishana tu ili tujuwe kama tutaendelea kuzivaa ama tuziweke kapuni.
No comments:
Post a Comment