Ama kweli nimeamini Maisha ni Watu na siku zote Tenda Wema Nenda zako.
Huyo
 jamaa  aitwae Bondia Mada Maugo maskani yake Gongo la Mboto.Jana 
alikuwa na Uzinduzi wa Wimbo wake aloimbiwa na Bendi ya Kijaluo.
Nilienda
 hapo kumsapoti mpaka nikanunua CD 1 kwa SH 50000.Yote hayo ni kwa ajili
 ya kumpa yeye Sapoti na hata hivyo mimi huwa nampa sana sapoti 
anapokuwa na mechi zake pamoja na kuwa anaishia kutwangwa,ila kumbe 
fadhila za Punda ni Mateke.
STory
 iko hivi,jana baada ya Uzinduzi wa hiyo CD wakati wa kuondoka Dem wake 
tena akiwa na Yeye Maugo akaja kuongea na mimi akidai anasoma Chuo Cha 
Utangazaji hivyo angefurai kama ningempa sapoti ya kufanya fild TBC fm 
na akadai anapenda  Sana Vipindi vyangu hivyo lets be intouch.
Akiwa
 anazungumza na mimi alikuwa akiongea kiingereza,sasa sikujua labda Mada
 alijua Dem wake ananitaka au la.Si unajua tena Mwenzangu na mimi hajui 
hata ya kuombea maji,hiyo lugha imempita kushoto.
Jamaa akaanza kufoka na kuanza kumpiga Dem wake,Akaona haitoshi Kachukua sime kwa gari eti anakuja kunichoma nayo.
Bahati
 nzuri kulikuwa na Watu pale Wakamshika.Ila Poa Pamoja na yote mimi kwa 
Roho Safi nimemsamehe coz yule mtu na Chizi hakuna utofauti.Ngumi 
anazopigwa zimemfanya awe Chizi.Kwa Wanaomjua Vizuri watakubaliana na 
mimi.
Vituko anavyofanya mtaani Ni noumah sana!!
SOURCE-DJARO 
 

 
No comments:
Post a Comment