Kama
mwenyekiti mtendaji wa record label aliyewakataa Beatles, kulikuwepo na
mkuu wa masoko aliyekuwa akifanya kazi na RIM (sasa hivi BlackBerry)
aliyeichezea siku aliyosikia jina "Justin Bieber".
Kwa
mujibu wa jarida Bloomberg BusinessWeek, Bieber aliifuata kampuni hiyo
mwaka 2007 (kipindi ambacho hakuwa maarufu) na kuwaomba awe balozi wao
(brand ambassador).
Aliyekuwa Meneja Mkuu wa maendeleo ya biashara wa RIM alisimulia:
“Kitu
kimoja tulichokikosa kilikuwa kwamba Justin Bieber alitaka kuwa
mwakilishi wa BlackBerry. Alisema: Nipeni $200,000 na simu 20 na
ntakuwa balozi wenu. Tuliwapelekea wazo watu wa masoko na kuwaambia:
Huyu ni mtoto wa Canada, alikulia hapa, watoto watapenda.
Walitufukuza
na kusema ‘huyu mtoto ni wa muda. Hawezi kufika popote. Na mimi kwenye
mkutano niliwaambia ‘huyu mtoto atadumu zaidi ya RIM.” Kila mmoja
alicheka.
Of course, mwaka 2013 RIM walibadili jina na kuwa BlackBerry. Bieber … bado anaitwa Bieber.
Kipindi
hicho kampuni ilikuwa hata haifanyi matangazo kwakuwa umaarufu wake
kwenye biashara uliwapa kiburi kuwa watu wangenunua tu simu. Mambo
yalianza kuwa magumu kwa Blackberry baada ya simu iPhone na zinazotumia
mfumo wa Android kushika kasi.
Mwaka
huu pekee, kampuni ya Blackberry imepoteza dola bilioni 1 kwa miezi
mitatu pekee. Kwa miaka mitano iliyopita, thamani ya kampuni hiyo
imeshuka kwa asilimia 85 hadi kufikia dola bilioni 4 kutoka dola
bilioni 80 mwaka 2008.
Mwaka
2013, kampuni ya Fairfax ilitoa ofa ya kuinunua BlackBerry kwa dola
bilioni 4.7. Mwezi September, kampuni ilitangaza kuwaachisha kazi
wafanyakazi 4,500.
Wakati
huo huo, Justin Bieber ameendelea kupeta. Kwa sasa ana utajiri wa
$130million,na amekamata nafasi ya 9 ya Forbes ya mastaa wenye ushawishi
zaidi duniani.
Pole yao Blackberry.
No comments:
Post a Comment