 Je ni kweli Steven Kanumba ameondoka na Kila kitu?
Je ni kweli Steven Kanumba ameondoka na Kila kitu?
Tangu Alipofariki Tasnia ya filamu Tanzania ni kama imelala usingizi wa 
Pono, Potelea mbali hata kama kuna watu bado wanaingiza mamilion ya pesa
 lakini ukweli ni kwamba mvuto wake unaendelea kupotea ..Nani anabisha?
Kwa kudhihirisha hilo Tazama wasanii wa kike wanavyojiingiza kwenye fani
 zingine zinazolipa ..Hawataki tena kupaka poda za location bali 
wanataka kukata viono kama Ray Majukwaanii...Mabadiliko na Maisha ya 
Shilole na Snura ni Mfano Tosha kabisa..
Kanumba alikuwa ni kila kitu biashara ya Filamu ilifanyika kupitia 
yeye..mzunguko wa soko uliundwa kupitia kanumba..Alisafiri kutoka 
mashariki kwenda magharibi, kaskazini na kusini kwa sababu ya tasnia ya 
filamu tu hakuwa akisafirisha Unga wala Pembe za ndovu..
Hivi sasa wasanii wa filamu hawavumi kupitia kazi zao, Ukimtazama mtu 
kama Ray utagundua kazi zake zilikuwa zinavuma kwa msukumo wa Ray lakini
 sasa zote chali ...Sasa anavuma kwa kugonganisha vimwana badala ya 
kuingiza movies mpya mtaani...
Kinacho Imaliza Bongo Movies kwa sasa ni Ubinafsi, Haraka , Mipango Butu na Tamaaaaa....
 
 
No comments:
Post a Comment