Bomu limeokotwa karibu na eneo la Kanisa la Huduma ya Maombezi ambalo
pia ni eneo la makazi ya watu katika barabara ya Barakuda Kata ya
Mazimbu Manispaa ya Morogoro.
Bomu hilo liliokotwa juzi asubuhi na mtoto ambaye alikuwa akilima
bustani jirani na nyumba yao na baada kuchimbua udongo aliona kitu
kizito na kukitoa.
Mmoja mashuuda, Brayton Sospeter, alisema bomu hilo liliokotwa na mtoto
huyo na baadaye kulichukua na kwenda kuwaonyesha watoto wenzake
waliokuwa wakicheza katika eneo hilo.
Alisema watoto hao waliendelea kulichezea
na baadaye kumuonyesha mzee mmoja liyekuwa akipita katika eneo hilo na kugundua kuwa ni bomu, hivyo kutoa taarifa Polisi.
Sospeter alisema baadaye Polisi walifika katika eneo hilo na
kuthibitisha kuwa ni bomu na kueleza kuwa ni kubwa hivyo hawana uwezo wa
kulitoa katika eneo hilo na badala yake walizungushia uzio huku
wakiahidi kwenda kuwasilina na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa
ajili ya kulitoa katika eneo hilo.Hata hivyo wanajeshi hawakufika.
Naye mmoja wa waumini wa kanisa hilo, alijitambulisha kwa jina la mama
Maloda, alilalamikia vyombo vya usalama kutoliondoa licya ya
kuthibitisha kuwa ni bomu.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, John Laswai, alithibitisha
kuwepo kwa taarifa hizo na kwamba walikuwa wakiwasilina na JWTZ ili
kwenda kulitambua.
Hadi jana mchana, bomu hilo liliendelea kuwapo eneo hilo bila JWTZ kufika.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment