Misa ya kitaifa ya wafu kumuaga Hayati Nelson Mandela, inaendelea mjini Johannesburg Afrika Kusini. Rais
 wa Marekani Barack Obama na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
 watakuwa miongoni mwa viongozi wa dunia watakaohutubia muhadhara huo.
 Rais
 wa Marekani, Barack Obama na Mke wake wakisoma kitabu cha ratiba ya 
misa ya kumuombea rais wa zamani wa Afrika ya Kusini  Nelson Mandela 
aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95.
 Mke
 wa Marehemu, Graca Machel akiwa kwenye hali ya uzuni wakati wa misa ya 
kumuombea marehemu Nelson Mandela aliyekuwa rais wa zamani wa Afrika ya 
kusini.
 Viongozi hao pia watahutubia wananchi sawa na wajukuu wanne wa Mandela . Maelfu ya watu wamehudhuria misa hiyo katika uwanja wa FNB. Afrika
 Kusini imeandaa shughuli mbali mbali za kumuenzi Mandela kabla ya siku 
ya kuzikwa kwake nchini Afrika Kusini siku ya Jumapili. Misa ya leo ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya viongozi wa kimataifa iliyoshuhudiwa nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.
 Rais
 wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma alipowasili kwenye uwanja First 
National Bank (FNB) kwa ajili ya maombezi ya mwili wa rais wa zamani wa 
Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela
Misa hiyo itafanyika katika uwanja ambako Nelson Mandela alionekana kwa mara ya mwisho hadharani. Misa hiyo itaonyeshwa kwenye skrini kubwa nje ya uwanja ili kuzuia msongamano wa watu. Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95 na kwa wengi yeye ni shujaa na mkombozi wa Afrika Kusini
 Rais
 wa Brazil Dilma Rousseff (kulia) akiwasili kwenye uwanja wa First 
National Bank (FNB) kwa ajili ya maombezi ya mwili wa rais wa zamani wa 
Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela
Viongozi wengine Watakaohudhuria misa ya wafu ya Mandela: Watu
 wengi wamekaidi hali mbaya ya hewa ambapo mvua kubwa imenyesha huku 
wakikusanyika uwanjani humo wakisubiri kwa muda mrefu kabla ya misa hiyo
 kuanza muda mfupi uliopita. Waliohudhuria
 misa hiyo wamesemekana kuwa wenye furaha wakiimba nyimbo na kutaja jina
 la Mandela kwa shangwe unaweza kudhani ni mkutano wa kisiasa.
Mjukuu
 wa rais wa zamani,  Mandla Mandela akiwa kwenye uwanja wa First 
National Bank (FNB) kwa ajili ya maombezi ya mwili wa rais wa zamani wa 
Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela
PICHA NA YAHOO NA HABARI NA BBC SWAHILI
 





 
No comments:
Post a Comment