TP
Mazembe tayati imetua mjini Tunis, Tunisia kwa ajili ya Fainali ya
kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Sfaxien kesho
ikiwa na washambuliaji wawili wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally
Samatta na Thomas Emanuel Ulimwengu. Ulimwengu na Samatta waliicheza
Tanzania, Taifa Stars Jumanne mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe
ulioisha kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
baada ya mechi wakaenda kuungana na klabu yao iliyokuwa kambini
GhanaBaada ya wiki moja ya kambi yake Lizzy Sports Complex mjini Accra,
Mazembe iliondoka Jumatano asubuhi na kutua jioni Tunis. Baada ya safari
ya saa nne (4) na dakika 45 kwenye ndege, waliwasili Uwanja wa ndege wa
Carthage mjini Tuni
Baada ya
kuwasili, Robert Kidiaba na Cheibane Traore pamoja na kocha Patrice
Carteron walijibu maswali ya Waandishi wa Habari wa Tunisia kabla ya
timu kwenda kupumzika hotelini kwa dakika 30 kisha kwenda kufanya
mazoezi.
Sfaxien,
timu pekee iliyoshinda Kombe la Shirikisho mara mbili tangu
kutambulishwa kwa mfumo mpya mwaka 2004, maskani yake ipo katika mji
uliozungukwa na bahari ya Mediterranean, Sfax.
Mechi ya
marudiano itachezwa mjini Lubumbashi, DRC Jumamosi ijayo, ya Novemba 30
na mshindi atajinyakulia kitita cha dola za Kimarekani, 625 000 wakati
mshindi wa pili atapata dola 432 000.
Mshindi
pia atamenyana na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Al Ahly ya Misri kuwania
taji la Super Cup mechi itakayopigwa nchini Misri Februari 2014.
Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment