Kwa kumaanisha kuwa hataki kutoka na staa huyo, Lulu alilazimika kubadilisha namba ya simu yake ya mkononi ili kuepuka usumbufu kutoka kwa bwana mdogo huyo ambaye kila kukicha amekuwa akiwindwa na wasichana warembo ili tu waonje sukari yake.
Pia inasemekana lengo la diamond kutaka kutoka na Lulu ni kutaka kukuza jina lake(kiki) kwa kuwa anaamini staa huyo ana jina kubwa na lenye mvuto hivyo kumfanya na yeye aogelee kwenye dimbwi la umaarufu na kuongelewa zaidi na watu,na kuwa ishu iyo ndo itakuwa habari ya mujini yaan yeye kutoka na lulu.
Baadhi ya watu wameonyesha kushangzwa sana na msimamo mkali wa binti huyo,kwa kuwa waliamini hakuna staa yeyote bongo mwenye ubavu wa kupindua kwa diamond,kama ilivyokuwa kwa Wema,Jokate,Aunt,Wolper na baadhi ya mastaa ambao dogo huyo aliwamega kiulaini.
Watu wanahaha kumjua mwanaume anayempa jeuri Lulu hadi kufikia hatua ya kuchomoa kwa diamond.
No comments:
Post a Comment