MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Rutamba, Wilaya ya Lindi
amekutwa akiwa na nguo za ndani pekee katika usingizi mzito kwenye kibao
cha shule hiyo huku akiwa hajitambui kwa madai ya kilichomkutana
kinahusishwa na imani za kishirikina.
Tukio hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi
mmoja wa kijiji hicho, Juma Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye
kibao hicho wakati alipokuwa anamsindikiza nduguye,Aisha Mbilimoto
aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar es Salaam.
Akizungumzia tukio hilo, shuhuda huyo alisema
alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala chini ya kibao cha shule akiwa na
nguo ya ndani tu (chupi)huku akikoroma kutokana na kuwa na usingizi
mzito.
Alisema awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua jukumu la kumwamsha ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka kwenda nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwa
Alisema awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua jukumu la kumwamsha ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka kwenda nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwa
Kwa upande wao walimu wa shule hiyo walisema kuwa,
wamekosa molari wa kufanya kazi kutokana na kitendo alichofanyiwa
mwalimu mwenzao.
Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake mwalimu wa
taaluma wa shule hiyo, Francis Milanzi alisema walimu shuleni hapo
wamekosa amani na kuwasababishia kuzihama nyumba zao kwa muda na badala
yake kwenda kukesha kwenye ofisi za walimu tangu tukio hilo litokee.
Ofisa elimu wa Wilaya ya Lindi, Cosmas Magigi
alisema amepokea taarifa za tukio hilo kwa huzuni na amewaomba walimu
kuwa na subira wakati utaratibu wanalishughulikia suala hilo.
Magigi aliongeza kuwa ofisi yake itafanya
utaratibu wa kumhamisha mwalimu huyo na kumtafutia shule nyingine huku
akiwataka wakazi wa eneo hilo kujenga ushirikiano na watumishi ili
waweze kutekeleza majukumu yao.
CHANZO: MWANANCH
No comments:
Post a Comment